Utumiaji wa methali katika insha - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Semi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=49) +---- Thread: Utumiaji wa methali katika insha (/showthread.php?tid=717) |
Utumiaji wa methali katika insha - MwlMaeda - 08-01-2021 Utumiaji wa methali katika Insha Ni vizuri mwanafunzi aelewe kwamba, katika insha methali hutumika kwa njia mbili: i) kuonyesha mhusika aliyazingatia mafunzo ya methali. ii) kuonyesha mhusika aliyapuuza. Uangalie mfano ufuatao: Mhusika fulani alikuwa na bidii katika shughuli zake. Katika mfano huu, tunaweza kutumia methali mchumia juani huliakivulini kuonyesha aliizingatia methali hii. Iwapo mhusika alikuwa mzembe bado tunaweza kuitumia methali hii huku tukionyesha aliipuuza.
Semi za kutumia pamoja na methali
|