MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

Chemsha Bongo - Printable Version
|
Chemsha Bongo - Printable Version
+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6)
+---- Forum: Semi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=49)
+---- Thread: Chemsha Bongo (/showthread.php?tid=715)
|
Chemsha Bongo - MwlMaeda - 08-01-2021
Chemsha Bongo- Maswali ambayo huhitaji mtu kutumia akili na ujuzi kuyajibu.
- Mafumbo ni kauli zenye maana iliyofichika na hujumuisha vitendawili na chemshabongo.
Mifano
- Kilo moja ya chuma na kilo moja ya nyama ipi nzito?
- Amada ana wafanyikazi saba, wanne hufanya kazi vizuri, wawili ni kama wamekufa, mmoja ni kama mwenda wazimu- miguu, pembe na mkia wa ng’ombe.
- Kipungu alipita juu, mama na ndege wawili wakamwangalia. Je macho mangapi yalimuona kipungu?- manne.
- Nina watu wangu watatu, wawili ni watoto na wawili ni baba- mtoto, baba na babu.
- Chura alitumbukia katika shimo la futi 30 na anaruka futi 10. Aruke mara ngapi ili atoke?- Hawezi.
- Watu watatu wanavuka mto. Mmoja aliyaona maji na kuyakanyaga. Wapili aliyaona lakini hakuyakanyaga. Watatu hakuyaona wala kuyakanyaga. Watu hao ni kina nani?
Sifa
- Ni kauli fupi au ndefu.
- Hutuia lugha ya kimafumbo.
- Hutumia ufananisho wa kijazanda.
- Huhitaji mtu kuwaza ili kupata jibu.
- Hujengwa na vitu vinavyotokana na mazingira.
- Hazina muundo maalum kama methali, nahau na vitendawili
- Hupima uwezo wa msikilizaji wa kutambua jambo lililofichwa.
Umuhimu
- Kuimarisha stadi ya kusikiliza.
- Kunoa uwezo wa kufahamu.
- Kutoa mawaidha.
- Kufunza kuhusu maumbile.
- Kuimarisha uwezo wa kukumbuka.
- Kufunza mambo kuhusu mazingira na maumbile.
- Kukuza uwezo wa kutumia lugha.
- Kukuza uwezo wa kufikiri.
- Kuburudisha na kuchekesha.
- Kukuza uwezo wa kubuni.
|