NAHAU ZA KISWAHILI NA MAANA ZAKE [TRANSLATED SWAHILI SAYINGS] - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Semi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=49) +---- Thread: NAHAU ZA KISWAHILI NA MAANA ZAKE [TRANSLATED SWAHILI SAYINGS] (/showthread.php?tid=713) |
NAHAU ZA KISWAHILI NA MAANA ZAKE [TRANSLATED SWAHILI SAYINGS] - MwlMaeda - 08-01-2021 NAHAU ZA KISWAHILI NA MAANA ZAKE [TRANSLATED SWAHILI SAYINGS] Imenukuliwa kutoka Gazeti la HABARILEO, Tanzania la Alhamisi, Januari 8 – 14, 2015 Na GENOFEVA MASAOAmekula chumvi nyingi – Ameishi miaka mingi [lived a long life] Ahadi ni deni – Timiza ahadi yako [be trustworthy; keep your promise] Amewachukua wazee wake – Anawatunza vizuri wazazi wake [taking good care of parents] Amekuwa popo – Yu kigeugeu [ a turncoat] Amevaa miwani – Amelewa pombe [chakari] [inebriation, a drunkard] Amekuwa mwalimu – Yu msemaji sana [a talkative person] Amemwaga unga – Amefukuzwa kazi [ dismissed from employment] Ana ulimu wa upanga – Ana maneno makali [biting words] Ameongezwa unga – Amepandishwa cheo [promoted] Agizia risasi – Piga risasi [shoot!] Chemsha bongo – Fikiri kwa makini [think analytically] Kuchungulia kaburi – Kunusurika kifo [saved from a worse fate] Fyata mkia – Nyamaza [keep silent] Fimbo zimemwota mgongoni -Ana alama ya mapigo ya Fimbo mgongoni [birching scars on ones’ back] Hamadi kibindoni – Akiba iliyopo kibindoni [savings for a rainy day] Hawapikiki chungu kimoja -Hawapatani kamwe ! [always at loggerheads] Kupika majungu – Kufanya mkutano wa siri [conspire a secret meeting] Kumpiga [kumvika] kilemba cha ukoka – Kumsifu mtu kwa unafiki [kinafiki] [paying lip service] Kula mlungula – Kula rushwa [receiving a bribe] Kupelekwa miyomboni – Kutiwa [kupelekwa] jandoni [performing circumcision] Kujipalia mkaa – Kujitia matatani [get yourself in trouble] Kumeza [zea] mate – Kutamani [to crave for] Kumuuma mtu sikio – Kumnong’oneza mtu jambo la siri [tell a secret to someone] Kumpa nyama ya ulimi -Kumdanganya mtu kwa maneno matamu [using wiles to tell lies] Kumchimba mtu – Kumpeleleza mtu siri yake to dig one’s secrets] Kutia chumvi katika mazungumzo – Kuongea habari za uwongo [tell lies] Vunjika moyo – Kata tamaa [give up] Yalimkata maini – Yalimtia uchungu [emotional pain] Kujikosoa – Kujisahihisha [correct your ways] Kutia utambi – Kuchochea ugomvi [convince someone to fight] Kumeza maneno – Kutunza siri moyoni [to keep a secret] Kula njama – Kufanya mkutano wa siri [to conspire a secret meeting] Kumkalia mtu kitako – Kumsema/kumsengenya [to talk about someone] Kupiga vijembe – Kumsema mtu kwa fumbo [use idioms to talk about someone] Kiinua mgongo – Malipo ya pongezi/uzeeni [pension] Kazi ya majungu – Kazi ya kumpatia mtu posho [hand to mouth existence] Kaza kamba – Usikate tamaa – [never give up!] Kumwonyesha mgongo – Kujificha – [to hide] Kuona cha mtema kuni – Kupata mateso [torture] Maneno ya uwani – Maneno yasiyo na maana/porojo – [hyperbole !] Mate ya fisi – Kata tamaa kupita kiasi – [give up totally !] Mbiu ya Mgambo – Tangazo [advertisement] Mungu amemnyooshea kidole – Mungu amemuadhibu – [God’s punishment] Mkubwa jalala – Kila lawama hupitia kwa mkubwa – [The eldest is the Dumping ground!] Mkaa jikoni – Mvivu wa kutembea – [a stay at home person] Mungu si Athumani – Mungu hapendelei [God is fair] Ndege mbaya – Bahati mbaya [bad luck] Paka mafuta kwa mgongo wa chupa – Danganya [telling lies] Usiwe kabaila – Usichume tokana na jasho la mwingine [Don’t exploit others] Usiwe kupe – Fanya kazi [be gainfully employed] Usiwe bwanyenye – Usichume kwa vitega uchumi vyako [don’t be a capitalist!] Usiwe na mrija – Usinyonye wenzako [don’t be exploitative] Utawala msonga – Utawala wa wachache [leadership of the few] Usiwe nyang’au – Usidhulumu kwa kutumia madaraka [Don’t use your position to exploit others] usiwe Kikaragosi – Usiwe chui katika ngozi ya kondoo [Don’t be a sheep in a leopard’s skin] Umangimeza – Viongozi wanaopenda kuamrisha watu [a Dictatorship] Kutoa ya mwaka – Kufanya jambo zuri na la pekee [performing a unique act] Kumpa mtu ukweli wake – Kumwambia mtu wazi [to be transparent] Pua kukaribiana kushikana na uso – Kukunja uso kwa hasira [to express anger] Sina hali – Sijiwezi [I am helpless (mostly when talking about love)] Kupiga uvivu – Kukaa tu bila kazi [abject laziness] Kupiga kubwa – Kwenda moja kwa moja [vanishing act] Kumwekea mtu deko – Kulipiza kisasi [pay back] Mtu mwenye ndimi mbili – Kigeugeu [A turncoat] Miamba ya mitishamba – Wanga hodari wa kienyeji [ expert wizardry] Kupiga supu – Tegea [do the least] Kupiga mali shoka – Gawana [distribute (contraband, bullion, inheritance] Kula vumbi – Pata taabu [struggle] Mafungulia ng’ombe – Kati ya saa mbili na saa tatu [between 8.00 and 9.00 o’clock Kutia kiraka – Fichia siri [confiante] Kumlainisha mtu – Kumzungumzia mtu maneno matamu mpaka akubali matakwa yako [convince someone to see eye to eye – to agree to your argument] |