NADHARIA YA UHUSIANO: AINA ZA PROPOSISHENI (3) - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Nadharia mbalimbali (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=14) +--- Thread: NADHARIA YA UHUSIANO: AINA ZA PROPOSISHENI (3) (/showthread.php?tid=617) |
NADHARIA YA UHUSIANO: AINA ZA PROPOSISHENI (3) - MwlMaeda - 07-23-2021 AINA ZA PROPOSISHENI
Fleming (1988:53-57)
anasema kuwa proposisheni ni za aina tatu ambazo ni: Proposisheni ya hakika, proposisheni ya thamani na proposisheni ya sera. Sehemu hii inadhamiria ama kuorodhesha aina za proposisheni. Inafuatwa na mjadala kuhusu aina hizi za proposisheni na hatimaye tutatoa mifano kwa kila mojawapo. Proposisheni ambazo tutazichanganua ni kama zifuatavyo: PROPOSISHENI YA HAK1KA
Proposisheni hii ni
tamko ambalo hulenga hasa katika imani ya msikilizaji, kama ni ya kweli ama ni ya uongo. Jinsi itakavyojadiliwa ndivyo itakavyoibua namna msikilizaji atakavyoichukulia kuwa ni ya kweli au uongo. Mfano huu hapa chini utatoa mwangaza zaidi. Kwa mfano: ‘ Vyuo vikuu vyole hupatikana mjini Tamko hili litategemea jinsi msemaji atakavyoinshawishi msikilizaji. Kama msikilizaji hana mfano wowote wa Chuo Kikuu anachokijua kuwa mjini, basi atakubali kuwa proposisheni hii ni ya kweli, lakini kama anakijua Chuo Kikuu chochote ambacho hakimo mjini basi kwake proposisheni hii itakuwa ni ya uongo. Proposisheni katika mfano, ni: 1)
Msemaji anamaanisha kuwa vyuo vikuu havipo mahali pengine ila katika miji tu. 2)
Huenda ikawa msemaji anataka kumsawishi msikilizaji kuwa kauli hii ni ya kweli. 3)
Labda msikilizaji hana ufahamu wa kutosha kuhusu vyuo vikuu. Vilevile, katika mfano
mwingine unaoafikiana na huu. Kwa mfano: ‘ Wanaume wote ni wabaya’.
Kauli kama hii
itategemea mtazamo wa watu mbalimbali. Kuna wale wanao amini ilhali wengine wanakataa. Pia itategemea ushawishi kutoka kwa msemaji kuhusu tajriba yake ikilinganishwa na tajriba aliyonayo msikilizaji kuwahusu wanaume, kisha ataweza kuamua kauli kama hii inajambo ambalo ni la kweli au la ni jambo la uongo. Huenda ikawa msemaji amekabiliwa na janga fulani lililo sababishwa na mwanamume ilhali, msemaji hajawahi kupatwa na jambo lolote baya kutoka kwa mwanamume yeyote. Proposisheni katika mfano,
ni kuwa: 1)
Msemaji anajumlisha wanaume wote kuwa ni wabaya. 2)
Msemaji labda ana sababu ya kusema jambo hili. 3)Msemaji
anonekana kuwa na hasira. PROPOSISHENI YA THAMANI
Proposisheni hii ni
tamko ambalo msemaji hutoa ili kutaka kupata maoni ya kutathmini kama tamko lake ni nzuri kimaadili au la, ni sawa au si sawa. Msikilizaji hasa hulinganisha vitu viwili na kuuliza ni kipi kilicho bora zaidi. Kwa mfano: ‘Kuna mwanafunzi anayekula darasani, ilhali
wengine wanamsikiliza mwalimu’. Proposisheni katikamfano,
ni kuwa: 1)
Kuna wanafunzi walio darasani. 2)
Kuna mwalimu ambaye anafunza katika darasa hilo. 3)
Mwalimu anapofunza kuna mwanafunzi mmoja ambaye yuala katika darasa hilo. Kauli hii itategemea
maoni ya msikilizaji ambaye katika proposisheni anayoifahamu ni maadili mema kumsikiliza mwalimu darasani badala ya kula. Mwanafunzi anafahamu kuwa si sawa kula darasani kama mwalimu anafundisha, lakini labda analifanya jambo hili kwa kusudi fulani. Hivyo basi, wasikilizaji wataamua ni jambo lipi lililo bora zaidi ya lingine. Vilevile, mfano mwingine wenye kueleza jambo lililo sawa na hili. Kwa mfano: ‘Kuna mtu anqyepiga gumzo kanisani ilhali
Padre anahuhiri.’ Proposisheni katika
mfano, ni kuwa: 1)
Kuna wakristo walio kanisani kwa ibada. 2)
Kuna mtu mmoja ambaye anazungumza ndani ya kanisa. 3)
Padre anaendelea na shughuli ya ibada huku mtu fulani akipiga gumzo. Vilevile kauli kama hii
itategemea maoni ya washiriki katika mjadala kama huu. Watu wasio mcha Mwenyezi Mungu hawataliona kuwa ni jambo baya kufanya kitendo kama hiki. Kwingineko, wanaomheshimu Mwenyezi Mungu watachukulia kuwa ni dhambi. Hivyo basi, ubora wa tendo kama hili utategemea mitazamo ya watu walio na tajriba tofauti kuhusu maisha. PROPOSISHENI YA SERA
Proposisheni hii ni
tamko ambalo hutoa mawazo kuhusu jambo litakalofanywa kama hatua ifaayo. Msikilizaji hupaswa kupitisha sera mwafaka au kujitolea kwa tendo maalum. Kwa mfano: ‘Mtuyeyote atakayepoteza kitabu alichokiazima
atanunua kingine ’. Kauli hii ni kulingana
na sera iliyopangwa na wahusika. Hivyo basi, kauli hii, ina proposisheni kuwa: 1) Kila mmoja wao amekubali tendo maalum la kununua kitabu
atakachokipoteza. 2)
Kuna vitabu ambavyo huazimwa mahali pale. 3)
Kuna masharti fulani ambayo ni lazima yazingatiwe kuhusu kitabu kilichoazimwa. Vilevile, hakuna mtu
yeyote ambaye ataepuka hatua hii kwa sababu yajumlisha watu wote. Kwingineko, katika mfano: ‘Mwanafunzi yeyote atakayechelewa kuwasili shuleni atarudi nyumbani’ Proposisheni katika mfano,
ni kuwa: 1)
Mahali pale ni shuleni. 2)
Kuna wanafunzi ambao huhudhuria shule ile. 3)
Kuna sheria fulani ambazo lazima zizingatiwe kuhusu kuchelewa shuleni. Sera iliyopo katika
shule hii na baadhi ya shule ni kuwa mwanafunzi yeyote anapaswa kuwasili
shuleni kabla ya wakati uliovvekwa kama sheria au mara tu wakati huo
unapowadia. Atakayefanya kinyume na haya basi ataadhibiwa kwa kuambiwa arudi
nyumbani ilhali, wenzake wataendelea na masomo siku hiyo. Hakuna mwanafunzi
yeyote ambaye ni bora zaidi ya wengine kuwa hataadhibiwa.
MAREJELEO
Abraham, S.
(1996). A Theory o f Structural Semantics’. Mouton and Company Publishers.
Akmajian, A. na
Wenzake. (2004) Linguistics. An lntrodution to Language and Communication. Fifth
Edition: MIT Press, Cambridge.
Atichi, A.R. (2004) The
Semantic Distinctiveness of Kenyan English: UON. Unpublished MA
Thesis.
Atoh, F.O. (2001)
Semantics Analysis of Dholuo Nowns: The Semantics Field Approach. UON.
Unpublished MA Thesis.
Blass, R. (1990)
Relevance Relations in Discource. A Study in Special Reference to Sissala:
Cambidge University
Press.
Brown, G. na Yule, G.
(1983) Discource Analysis: Cambridge University Press.
Bussman, H. (1996)
Route ledge Dictionary o f Language and Linguistics: International
Thompson Publishing
Company.
Cambridge (2008)
Cambridge Advanced Learners Dictionary. Cambridge University.
Carston, R. (2002)
Thoughts and Utterances. The Pragmatics of Explicit Communication. MA:
Blackwell Publishers
Ltd.
Comford, F. M. (1957)
Platos Theory o f Knowledge: Routeledge and Kegan Paul Ltd.
Crystal, D. (2003) A
Dictionary o f Linguistics and Phonetics. Fifth Edition. Oxford: Blackwell
Publishers.
Falsod, R. W. (2002) An
lntrodution to Language and Linguistics. Cambridge University Press.
Fleming, (1998) Google
Search. Powered by The Ultimate Programming Weblog. Sil
lntematinal: http://
worldnet Princeton. Edu/Pert/Webwn.
Fodor, J. D. (1997)
Semantics: Theories o f Meaning in Generative in Generative Grammar:
Harper and Row ,
Publishers.
Fretheim, A. (2000)
Pragmatic Markers and Propositional Attitude: John Benjamin Publishing
Company.
Green, G. M (1996)
Pragmatics and Natural Language Understanding. Second Edition:
Lawrence Erlbaum
Associates Publishers.
Greenbaum, S. na
Wenzake. (1985) A comprehensive Grammar o f English Language: Longman
Group UK Ltd.
Griffin, E. M (1991) A
First look at Communication Theory. Wheaton College: Me Graw- Hill,
Inc. Company.
Hofmann, T. R. (1993)
Realms o f Meaning: An Introduction to Semantics: Longman Group UK
Ltd.
Ifantidou, E. (2001)
Evidentials and Relevance. Volume 86: John Benjamin Publishing
Company.
Kamau, S. K. (2008) An
Analysis o f Truth Conditions in Pragmatics: Relevance Theory
A p p r o a c h . UON.
Unpublished MA Thesis.
Kasher, A. (1998)
Pragmatics. Critical Concepts. Volume V: Communication, Interaction and
Discourse: Routeledge
Publishers.
Katie, W. (2001) A
Dictionary o f Stylistics: Longman Group UK Ltd.
Katz, J.J. (1977)
Propositional Structure and Illocutionary Force. A Study of the contribution of
Sentence meaning and
Speech Acts: The Harvest Press.
Kempson, R. M. (1975)
Pressuposition and The Delimination o f Semantics: Cambridge
University Press.
Larson, M. L. (1984)
Meaning-Based Translation: A Guide to Cross-Language Eqivalence:
University Press of
America, Inc.
Leech, G. (1974)
Semantics: Penguin Books Limited.
Leech, G. N. (1971)
Towards a Semantic Description o f English: Longman Group Ltd.
Linsky, L. (1952)
Semantics and the Philosophy o f Language: University of Illinois Press.
Longmans (1968)
Longmans English Larousse: Longmans, Green and Co. Ltd.
Munga, C. M. (2009)
Sence Relations in Gikuyu: A Lexical Pragmatics Approach. UON
Unpublished MA Thesis.
Ndug’u, M. N. (2009)
Mada na Fokasi katika Kiswahili: Mtazamo wa Muundo wa Taarifa.
UON. Unpublished MA
Thesis.
Ogola, C. A. (2006) A
Pragmatic Analysis of Intercultural Communication Failures. UON,
Unpublished MA Thesis.
Palmer, F. R. (2006) An
Introduction to Language and Linguistics: Cambridge University Press.
Rouchota, V, na Jucker,
H. (1998) Current Issues in Relevance Theory: John Benjamin
Publishing Company.
Saeed, J. L. (2003)
Semantics. Second Edition: Blackwell Publishing Ltd.
Schroeder, H. (2005) Do
we Speak the same Language? A cognitive Pragmatic Explanation of
Cultural
Misunderstanding. In Across Borders: Benefiting from Cultural Differences.
Conference Proceedings.
17^-18th March: 2005.
Sperber, D na Wilson,
D. (1995) Communication and Cognition, 2nd Edition: Blackwell
Publishers.
Sperber, D na Wilson,
D. (2004) A Handout on Relevance Theory (1985-2002): Blackwell
Publishers.
Tuki (1990). Kamusi ya
Isimu na Lugha. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili: Educational
Publishers and
Distributors Ltd.
Tuki (2006)
English-Swahili Dictionary. Third Edition: Book Printing Services Ltd.
Chanzo>>>>>[url=http://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/bitstream/handle/11295/5896/njue,carolinew_uchanganuziwaproposishenikatikakiswahili:nadhariayauhusiano.pdf?sequence=1][/url]
|