MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI: NAKULAUMU - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
SHAIRI: NAKULAUMU - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6)
+---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50)
+---- Thread: SHAIRI: NAKULAUMU (/showthread.php?tid=433)

SHAIRI: NAKULAUMU - MwlMaeda - 07-04-2021

NAKULAUMU

Nalia nagaragara, mganga kaniarifu,
Haki sio masihara, nimepata hitilafu,
Jamani hii hasara, hayana kazi mapafu,
Ulonifunza sigara, tambua nakulaumu.

Vipi nifunike kombe, nisinene nijihini,
Wacheni mie nigombe, nitulie yamkini,
Tayari nina uvimbe, kwenye figo nalo ini,
Uliyenifunza pombe, tambua nakulaumu.

Ninaanzaje kuvunga, ati! Nifiche aibu,
Mkono nilomuunga, ona umeniadhibu,
Leo niko kama bunga, wanitesa uraibu,
Uliyenifunza unga, tambua nakulaumu.

Chini nimelala doro, kuamka sitamani,
Jamani giza totoro, kuona mbele sidhani,
Kooni ninakasoro, yanitesa saratani,
Ulonifunza ugoro, tambua nakulaumu,

Katu siwezi nyamaa, nikabakia na fumbo,
Kweli ulinihadaa, nikafuata mkumbo,
Ona sasa ni balaa, nina vidonda vya tumbo,
Ulonifunza miraa, tambua nakulaumu.

Mwisho shairi lifike, kwenu vijana wenzangu,
Lifanye muelimike, yasiwakute ya kwangu,
Ombi msihadaike, mkapita nyendo zangu,
Laitani laitani, watu mkawalaumu.

Mshairi Machinga,
mfaumehamisi@gmail.com,
+255716541703/752795964,
Dar es salaam, Kkoo.

RE: SHAIRI: NAKULAUMU - MwlKapinga - 07-05-2021

??? shairi nzuri sana japo linahitaji kauwezo ka kufikiria kidogo

RE: SHAIRI: NAKULAUMU - MwlMaeda - 07-23-2021

(07-05-2021, 07:45 AM)MwlKapinga Wrote: ??? shairi nzuri sana japo linahitaji kauwezo ka kufikiria kidogo

Kweli na ndiyo utamu wa ushairi ulipo