MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

Vidahizo vya Fani ya Ufundi Viatu - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
Vidahizo vya Fani ya Ufundi Viatu - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Kamusi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=70)
+--- Thread: Vidahizo vya Fani ya Ufundi Viatu (/showthread.php?tid=352)

Vidahizo vya Fani ya Ufundi Viatu - MwlMaeda - 06-29-2021

Vidahizo vya Fani ya Ufundi Viatu
Bb
bikariolezi ji wing dividers: bikari itumiwayo na mafundi, k.m., seremala, fundi viatu, n.k., kutengeneza violezo.

bikariolezi
Kk
kichopeko ji shoe horn: kifaa maalum kinachosaidia kuingiza mguu kwenye kiatu wakati wa kukivaa.

kichopeko
kidira ji cutting nipper: Kifaa cha kukata na kung’oa misumari.

kidira
kisuwembe ji rampat edger: kifaa mfano wa wembe ambacho hutumiwa kwa ajili ya kukatia ngozi.

kisuwembe
Mm
maleti mpira ji rubber mallet: nyundo kubwa ambayo kichwa chake ni mpira.

maleti mpira
mwega feleji ji iron rest: pande la chuma ambalo juu yake huwekwa kiatu wakati wa kugongwa misumari.

mwega feleji
Nn
ngoeko ji hook: kifaa cha kukamatia au kutolea ubaowayo kwenye kiatu.

ngoeko
Pp
panchi gezamguu ji wooden hole punch: ubao uliochongwa kulingana na nambari tofauti za miguu ya watu.

panchi gezamguu
panchi mzunguko ji revolving punch: chuma chenye meno ya kutobolea matundu kwenye ngozi.

panchi mzunguko
Rr
riveti ji eyelet: metali zenye vitobo zinazowekwa kwenye vitundu katika viatu, nguo, n.k.

riveti