JIFUNZE KOMPYUTA KWA KISWAHILI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Kiswahili cha Kompyuta (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=13) +--- Thread: JIFUNZE KOMPYUTA KWA KISWAHILI (/showthread.php?tid=29) |
JIFUNZE KOMPYUTA KWA KISWAHILI - MwlMaeda - 06-15-2021 Katika hatua hii ya kwanza utajifunza kuhusu kampuni ya Microsoft na historia fupi ya waanzilishi wake. Utajifunza sehemu kuu za kompyuta ambazo ni KIU (Kitengo kikuu cha uchakataji) au CPU (Central Processing Unit), Monita, puku, bodidota na printa. Mfululizo wa masomo haya utakujengea msingi wa kuanza kutumia kompyuta hasa matumizi ya programu za Microsoft ofisi kama vile Microsoft Word, Microsoft powerpoint, Microsoft publisher, Microsoft Excel n.k.
Mpaka mwisho wa somo hili utajua:
Kuhusu kampuni ya Maikrosofti
Kampuni ya Maikrosofti ni kampuni ambayo hutengeneza programu za kompyuta kwa ajili ya watumiaji wa kompyuta duniani kote. Ilianzishwa mnamo mwaka 1975 na Bill Gates kwa kushirikiana na Paul Allen. Programu ambazo hutengenezwa na kampuni hii ni pamoja na windows, Microsoft office (kama vile, Microsoft word, Powerpoint, Publisher n.k), internet exproler (Programu ya kuingilia katika mtandao wa intaneti), websaiti ya Microsoft ijulikanayo kama Microsoft Network (MSN) ambayo hutumika kuingilia kwenye mtandao wa intaneti n.k. Baadhi ya programu za Microsoft kama vile mfumo wa Window wa uchakatuaji (Windows operating system) huwa zimekwisha ingizwa mara mtu ananunuapo kompyuta. Mtu aweza kununua na kuingiza nyingine kulingana na uhitaji wake.
Maikrosofti Windows ni nini?
Microsoft Windows ni mfomu laini wa uchakatuaji (operating system) ambao ni wa msingi ambao hufanya kompyuta kufanya kazi na kuruhusu program nyingine nazo kufanya kazi. Aina za Windows zinazotumika ni Windows XP au Windows 7 na Windows 8.1 ambalo ni toleo la hivi karibuni
Microsoft ofisi ni seti (mkusanyiko) ya program ambazo hutumika katika kompyuta kuwawezesha watu kuandika dokumenti. Mfano Microsoft Word na Microsoft Excel ambayo hukuwesha kutengeneza mahesabu na majedwali na Microsoft PowerPoint ambayo hukuwezesha kuandaa mawasilisho (presentations).
Kwakuwa programu hizi hufanya kazi katika kompyuta, sehemu inayofuata inalenga kukupa ufahamu juu ya sehemu za kompyuta (hasa za nje) na zinavyofanya kazi.
Kuhusu waanzilishi wa kampuni ya Microsoft
Kampuni ya Microsoft ilianzishwa na marafiki wawili; William Henry Bill Gates na Paul Gardner Allen
William Henry Bill Gates alizaliwa tarehe 28/10/1955 huko Seattle, Washington Marekani. Bwana Bill Gates alianza kuonesha mapenzi makubwa kwa teknolojia akiwa na umri wa miaka 13 ambapo alianza kutengeneza pro
gramu za kompyuta. Kupitia ujuzi wake wa kutengeneza programu za kompyuta na ujuzi wa mikakati ya kibiashara yeye pamoja na rafiki yake Paul Allen walijenga biashara kubwa ya programu za kompyuta iitwayo Microsoft. Biashara hii hatimaye ilinfanya Bill Gates kuwa mmoja wa matajili wakubwa ulimwenguni. Alisoma katika Shule ya Lakeside kati ya mwaka 1967 na 1973 kisha akasoma katika chuo cha Harvard Mnamo mwaka 1973 mpaka 1975 Huko Marekani. Ana mke aitwaye Melinda Gates na watoto watatu; Jennifer Katharne Gates, Rory John Gates na Adele Gates.
Paul Gardner Allen ni mfadhili wa Kimarekani, mwekezaji na mbunifu. Huyu ni rafiki yake Bill Gates na mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Microsoft. Alizaliwa January 21, 1953 Katika mji wa Seattle, Washington Marekani. Alisoma katika shule moja na Bill Gates iitayo Seatle na baadae alijiunga na chuo kikuu cha Serikali cha Washington (Washington State University) ambapo hakumaliza masomo yake badala yake akakimbilia Boston ambapo alipata ajila katika kampuni iitwayo Honeywell. Baada ya hapo Bill Gates aliungana naye wakaiendeleza safari ya ubunifu na hatimaye wakaanza biashara kubwa ya program za kompyuta iitwayo Microsoft.
Sehemu za Kompyuta
Kompyuta ni mashine ya kieleroniki ya kuhifadhi na kuchanganua taarifa zilizoingizwa, kukokotoa na kuongoza mitambo. Kompyuta ni mashine yenye nduni (characteristic) mbili: kwanza inaingiza seti maalumu ya maagizo kwa kufuata utaratibu maalumu na pili inaweza kunafidhisha orodha iliyorekodiwa ya maagizo (programu). Kompyuta za kisasa ni za kieletroniki na kidijiti. Mitambo yenyewe, kama vile waya, transista, na sakiti inaitwa maunzingumu (hardware) na maagizo na data huitwa maunzilaini (software).
Kwakuwa si lengo la somo hili kufundisha ufundi wa kompyuta, sehemu hii itakuonesha seti ya kompyuta kwa nje, sehemu zake na jinsi zinavyofanya kazi. Kyompyuta inasehemu kuu zifuatazo;
Somo hili linasehemu ya pili ambapo utajifunza kwa undani sehemu za bodidota (keyboard) na kujifunza njia mkato za bodidota. Mpaka mwisho wa sehemu ya pili utakuwa uko tayari kutumia kompyuta na programu za Microsoft Ofisi. Mwisho utafanya zoezi la kivitendo ili kujipima kama somo hili la utangulizi umelielewa kabla ya kwenda katika masomo magumu zaidi.
|