Kutoka Ukerewe hadi Iramba: Historia, Maisha na Tabia za Wanyiramba na Wanyisanzu - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Historia ya makabila ya kibantu (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=15) +--- Thread: Kutoka Ukerewe hadi Iramba: Historia, Maisha na Tabia za Wanyiramba na Wanyisanzu (/showthread.php?tid=288) |
Kutoka Ukerewe hadi Iramba: Historia, Maisha na Tabia za Wanyiramba na Wanyisanzu - MwlMaeda - 06-26-2021 Uleyleani! Wajuzi wa hiyo salamu tayari wamekwisha kujibu “izaa uduu”. Katika siku zilizopita tumekuwa na mfululizo wa makala mbalimbali yanayotupa fursa kujua kuhusu Historia, Maisha na Tabia za makabila mbalimbali hususani huku kwetu katika mikoa ya Manyara, Singida, Arusha na Shinyanga pamoja na mikoa jirani na hii. Tuliweza kuangazia utamaduni wa Wairaqw na Wadatoga na leo tutamulika kuhusu Wanyiramba na Wanyisanza wanaopatikana katika wilaya ya Iramba (Sasa ni Iramba na Mkalama) mkoani Singida…..Kanyaga twende…
Kama zilivyo kwa jamii zingine za kibantu barani Afrika ambao walihamia Mashariki na Kusini mwa Afrika wakitokea Afrika Maghariki hususani nchi za Kameruni, Naijeria na Ghana wakipita misitu ya Kongo, Wanyiramba na Wanyisanzu walikuwa katika kundi mojawapo lililoelekea mashariki hadi maeneo ya Ziwa Nyanza (Victoria) hadi katika kisiwa cha Ukerewe kilichopo katika ziwa hilo kubwa zaidi barani Afrika. Japo haijulikani sababu hasa, kundi moja liliondoka kutoka katika kisiwa cha Ukerewe hadi Kisiwa cha Uzinza na kutoka hapo wakahama hadi maeneo ya Tabora ambako waligawanyiaka kundi moja likielekea kusini na inasemekana ndio waliokuja kuwa Wagogo na Wanyaturu huku kundi lingine likiendelea kuelekea Mashariki kupitia mlima Sekenke hadi Kisiriri.
Walipoanza kuitwa Wanyiramba na Wanyisanzu/Waihanzu
Wakaishi hapo Kisiriri kwa muda mrefu kabla ya kutokea ukame mkubwa sana uliosababisha njaa katika eneo hilo. Ili kukabiliana na tatizo hilo la njaa, watu hao walitumia mboa za majani za mlenda uliokaushwa zijulikanazo kama “ndalu” kama chakula kikuu. Kutokana na kula “ndalu” kwa mtindo wa kulamba, watu wa makabila mengine ya kibantu walivyowaona wakawaita “wenye kulamba” na baadaye likabadilika hadi kuwa “wenyilamba” hadi “Wanyiramba”.
Ikumbukwe kuwa hadi hapo Wanyisanzu na Wanyiramba walikuwa kabila moja na wote walifahamika kama Wanyiramba baada ya njaa hiyo.
Wanyisanzu/Waihanzu wahamia pori la Mkalama
Kundi moja likaamua kuondoka hapo Kisiriri hadi pori la Mkalama wakiwa na mifugo yao na familia zao na walipofika katika pori hilo ili kujilinda na wanyama wakali wakajenga nyumba na kuzungushia maboma ya miba maarufu kama “masanzu/mahanzu”. Baadaye baadhi ya Wanyiramba waliobaki Kisiriri nao waliamua kuondoka hapo na walipofika Mkalama wakawakuta wenzao wamezungushia nyumba zao kwa Maboma ya “masanzu/mahanzu” ndipo walipoanza kuwaita hawa ni wanyisanzu au waihanzu.
Wanyiramba na Wanyisanzu japo wanahistoria inayofanana na kwa mtu mgeni anaweza kudhani kuwa hakuna tofauti baina yao, lakini ukweli ni kuwa kuna tofauti kubwa sana baina yao.
Koo zao na Wanapopatikana
Wanyiramba
Hizi ni koo tano za Wanyiramba na wanapopatikana
Kwa upande wa Wanyisanzu, wao wana Koo nne tu
Ndugu msomaji wa Ohayoda, yapo mengi sana usiyoyafahamu kuhusu makabila haya mawili yenye historia inayofanana na japo wanaishi pamoja na watu wengi kudhani ni kabila moja, wanatofauti kubwa sana hasa za tabia na mambo mengine kedekede. Katika Makala zijazo tutakujuza mengi hasa Lugha, Mofolojia/miili (Morphology), mavazi, tabia, miiko, matambiko, umiliki wa mali na chakula.
Usikose kufuatilia makala hii na zingine kuhusu mambo ya Utamaduni kila siku za Jumanne, Alhamisi na Jumamosi hapa hapa katika libeneke boooooora zaidi linalokujuza habari kemkem hasa za jamii halisi za Kitanganyika.
Kama una maoni, maswali au ushauri usisite kuwasiliana nasi au kuacha maoni yako hapo chini nasi tutayafanyika kazi ili kuboresha jamvi letu hili liwe na manufaa kwa wote.
Songela saana!
Mu hali gani wanaOhayoda popote mlipo duniani, leo nipo Kidarafa kijiji kilichopo katika wilaya ya Iramba (sasa Mkalama nadhani) kipo kilometa takriban 10 kutoka Haydom. Kidarafa kunanikumbusha mbali sana, kuna mlima maarufu sana unaitwa “Mlima wa Msalaba”, mlima ambao unajiwe refu juu yake na juu ya hilo jiwe kuna msalaba umewekwa. Sijui haswa historia ya huo msalaba na nani aliuweka na kwa nini, lakini Kidarafa inabaki kuwa sehemu muhimu ya maisha yangu ya utotoni. Hapo pia ndipo nilipoweza kufahamiana na kuishi na Wanyiramba na Wanyisanzu na wengi nilisoma nao nilipokuwa Shule ya Msingi Endaharghadatk.
Tuachane na hizo “story” za utotoni tutazipiga siku nyingine, kama kawa kama dawa, leo tunaendeleza tulipoishia juzi (Alhamisi) kuhusu Historia na Maisha na Tabia za Wanyiramba na Wanyisanzu, makala iliyopita tulipitia Historia yao na Koo mbalimbali na sehemu koo hizo zinakopatikana…ungana nami tuwafahamu hawa rafiki zangu ninapoandika makala hii kutoka Kidarafa pembeni ya “kata upepo”
SURA
Wanyiramba na Wanyisanzu wengi wana;
LUGHA
kama tulivyosema awali Wanyiramba na Wanyisanzu wote ni wabantu na lugha zao zimefanana kwa sehemu kubwa. Kwa mfano neno “twende” Wanyiramba husema “kweini” na Wanyisanzu husema “kweni”, Na MAJI Wanyiramba hutamka “Maazi” huku Wanyisanzu wakisema “Mazi”
Aidha zipo herufi za alfabeti za Kiswahili ambazo hazipo katika lugha hizi zote mbili. Mfano herufi “F”, “V” na “SH” hivyo maneno yenye hizo herufi hutamkwa kama ifuatavyo
Fimbo hutamkwa Pimbo
Ofisi wao husema Opisi
Viatu kwao ni Biatu
Ushanga wanasema Uchanga
TABIA
Hapa ndipo tofauti kubwa ilipo baina ya Wanyiramba na Wanyisanzu. Na moja ya tofauti kubwa ni kuwa Wanyisanzu ni moja ya jamii chache za Tanzania ambapo mwanamke ananguvu kuliko mwanaume (Matrilinier society) na mambo mengine kadha wa kadha
WanyirambaWanyisanzu Wanasalimia kwa sauti ya upole Wanasalimia kwa sauti ya Ukali Wanaetoa maelezo ya jambo hadi kieleweke (ni walimu wazuri na wavumilivu) Hutumia lugha ya ukali kuelekeza jambo na ni kama wanatoa maagizo Hutumia lugha ya kuomba na unyenyekevu Hawajui kuomba na hutumia amri Ni wakweli na hawajui kuficha siri Ni wasiri sana na hii hupelekea kutokuwa wakweli Hawapendi vita wala shari na watu wengine Wanapenda sana ugomvi Mwanaume ana madaraka ya mwisho katika familia Mwanamke ndiye mwenye mamlaka ya mwisho katika familia MIIKO
Kuna miiko mbalimbali katika jamii za kinyiramba na Kinyisanzu, hizi ni baadhi tu ya miiko yao japo mengi hayapo tena siku hizi za dot com
MYTH (Imani za “Kufikirika”)
Kuna wanyama huwa wanamikosi, kama ukiona paka wanajamiiana utaona au utasikia habari mbaya inayokuhusu, na kama kinyonga au mbweha akikatiza mbele yako wanaamini utasikia habari za kifo au ugonjwa wa ndugu yako
Mpenzi msomaji, naamini leo umepata machache ambayo ulikuwa huyajui kuhusu hawa ndugu zetu ambao wanapatikana katika Mkoa wa Singida hususani wilaya ya Iramba. Bado kuna mengi ya kujuzana kuhusu wao na jamii zingine za huku kwetu, hayo na mengine mengi yanakujia hapa hapa Ohayoda. Mpaka Jumanne ijayo ila usiache kusoma Ohayoda ujue mengi usiyoyajua
Songela Zig Zig
Na Amani Paul, Mwangeza
Kama tulivyoona katika makala mbili za awali kuhusu Historia, Maisha na Tabia za Wanyiramba na Wanyisanzu, leo tunaendelea na sehemu nyingine ambayo tutaangazia Mavazi na matambiko katika jamii hizi ambazo zinapatikana huku kwetu. Yapo mengi ya kujifunza na ambayo sisi tunajivunia kuwa na utajiri mkubwa wa utamaduni.
MAVAZI NA MAPAMBO
MATAMBIKO
Wanyiramba na Wanyisanzu wanathamini sana matambiko. Kuna matambiko ya mtu binafsi, familia, ukoo au jamii nzima. Kwa ajili ya matambiko, hutumia ngæombe mweusi aliyezaliwa usiku, mbuzi mweupe, kondoo mweusi, pombe na hori
Matambiko haya hufanyika kwenye mapango na makaburi na huwa kuna maeneo maalum ya kufanyia matambiko hasa kule Mwandu kwa Wanyiramba na kwa Wanyisanzu hufanyia matambiko yao kule Kirumi.
Wanyiramba na Wanyisanzu ni watumiaji wazuri w tumbaku hasa ugoro.
Pamoja na hayo niliyoyaeleza hapo juu, Wanyiramba na Wanyisanzu wamepoteza utamaduni wao kwa kiasi kikubwa sana hasa kutokana na mabadiliko ya maisha. Mambo mengi yamebadilika mfano
UMILIKI WA MALI
Ikumbukwe kuwa pamoja na kuwa Wanyiramba na Wanyisanzu wanahistoria inayofanana na tamaduni zao ni karibu sawa, lakini wanyisanzu wanautofauti pengine tofauti hii inawafanya wawe wa pekee zaidi yaani wanawake wananguvu zaidi ya wanaume (Matrilinear society). Kuna mali zinazomilikiwa na wanaume, wanawake, ukoo na jamii nzima.
Wanyiramba na Wanyisanzu wanasema kuwa “uzao ni kwa baba lakini ukoo ni kwa mama” wakimaanisha kuwa mwanaume anapooa ni sharti ahamie na kuishi kwa wake zake. Wakwe hawa wanawajibika kuwatunza pamoja na watoto wao kwa kuwapa chakula, shamba la kulima lakini hana haki na mapato yatokanayo na shamba hilo na kujengewa nyumba. Mwanaume huyo anapofariki urithi huenda kwa mjomba wake.
Siku hizi hali hii imebadilika kwa kiasi kikubwa na wanaume hawataki kwenda kuishi kwa wakwe ili kuondokana na dhana ya kuwa “ameolewa”
USHIRIKIANO NA JAMII NYINGINE
Wanyiramba na Wanyisanzu wamepakana na Wanyaturu kwa kusini, wasukuma upande wa magharibi, wahadzabe upande wa kaskazini na kwa upande wa mashariki wanapakana na Wairaqw na Wadatooga, ambao wamekuwa wakishirikiana katika nyanja mbalimbali kama ifuatavyo;
WANACHOPATA KUTOKA KWAWANACHOTOA KWA 1. Wairaqw: Chakula, punda na ng’ombe 1. Wairaqw: Mtama, mikuki, visu, tumbaku na ushanga na vibarua (wafanyakazi) 2. Wanyaturu: Watumwa (atugwa) kama malipo ya uganga wa mvua 2. Wanyaturu: Mtama, mikuki, visu, tumbaku na uganga wa mvua 3. Wahdzabe: Asali, Nyama, madawa ya asili na kuoleana 3. Wahadzabe: mtama, ushanga, tumbaku na kuoleana 4. Wasukuma: ng’ombe, uganga na kuoleana 4, Wasukuma: Ardhi, kibarua (nguvu kazi) na kuoleana 5. Wadatooga: mafuta, maziwa, ng’ombe na punda 5. Wadatooga: Tumbaku, ardhi na vibarua Mpenzi msomaji, ninaamini umeweza kujua kwa kiasi kikubwa kuhusu ndugu zetu hawa na yumkini ungependa kujua zaidi, kama una uswali, ushauri au maoni usisite kuwasiliana nasi. Nasi tutayafanyia kazi maoni yako au tutayajibu maswali yako hasa yanayohusu tamaduni za jamii mbalimbali.
Wasiliana nasi kwa kuacha maoni yako hapa chini au tuandikie barua pepe kupitia amanipaulit@gmail.com au nipigie kwa 0784238225!
Nikuache na utani wa huku Iramba kuwa “Iramba mukulu Tanzania kanino”
|