SHAIRI: NIMPENDE NANI ? - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: NIMPENDE NANI ? (/showthread.php?tid=2787) |
SHAIRI: NIMPENDE NANI ? - MwlMaeda - 07-22-2022 NIMPENDE NANI ? Mwenzenu nipeni rai kwa haya yalonifika Moyo wangu haukai, kwa hapa nilipofika Japo naona nishai, moyoni nimewatika Kati ya hawa wawili, Nipende nani zaidi? Huyu wa kwanza mpole , tena si muongeaji Kama simba mwenda pole, kwenye ufatiliaji Hutembea polepole ,amdake mwiwindwaji Kati ya huyu nayule jama nimpende nani? Huyu wa pili mweusi , kapanda juu kidogo Mwenye pua ya kitusi, mwili mwembamba kidogo Mtalamu wa kukisi,utadhania mgogo Kati ya huyu na yule ,jama nimpende nani? Akili inanituma , wa pili awe mwandani Ninategemea mema ,sitotoka asilani Kama ikiwa salama ,nitasota uvunguni Kati ya hawa wawili Nimpende nani? Nilikuwa na furaha,nimefika maskani Nikayaanza madaha, nikavipata vya ndani Nilishazika karaha,ninapokuwa chumbani Alivyokuja wa pili , Moyo wangu umeshindwa Wa pili yeye mcheshi , muda wote tabasamu Ni kweli kuwa achoshi ,twacheka kama binamu Kwangu hamu haiishi, jama mpeni salamu Kati ya Hawa wawili nimpende nani? Wa kwanza ananijali, kwa pesa nayo mahaba Nikimuuzi hajali, hunilea kama baba Na hunijulia hali, upendowe sio haba Wanagenzi mnijuze nimpende yupi? Rama karibu javini , unipe jibu murua Na wengine karibuni, jibu nataka kujua Nitomuweka moyoni, kofuli kumfungia Kitendawili tegua Yupi kwangu anafaa? DINNA ( MOM J ) 21/7/22 KUWA TAYARI KUHESABIWA MPE USHIRIKIANO KARANI WA SENSA?? |