SHAIRI: KUJUWA NI MATATIZO - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: KUJUWA NI MATATIZO (/showthread.php?tid=2598) |
SHAIRI: KUJUWA NI MATATIZO - MwlMaeda - 06-13-2022 KUJUWA NI MATATIZO Lugha yangu ya asili, niijuavyo si haba, najivuniayo sana Lakini hii ya pili, ni Kizungu chanikaba, uwelevu nayo sina Ndipo juzi Jumapili, akanitanza swahiba, tukaanza kuvutana Aliniambia: Silly!, nikadhani anshiba, kumbe yuwanitukana! Kuelewa ni kuzuri, hukukinga na kujuta, ukawa hutazozana Hukupunguza kiburi, ukadharau kuteta, ukapenda kushikana Ja vile kaka Saburi, alivyonitia tata, mpaka nikadangana Na nilipomshauri, aliponambia: Better, hapo hapo nikakona Si mjinga kama gude, huzitumia fikira, nawambia muelewe Bao latezwa kwa ndude, na kazi ni za majira, yakupasa uyajuwe Nenda skuli 'sidode, ujinga una izara, yasikufike na wewe Naliambwa: Hey dude!, nikajibu kwa hasira:, Na wewe dude mwenyewe! Kujiweka nyumanyuma, jambo hilo likataye, usiwatwe mkiani Utafanyiwa hujuma, wenzako wakukimbiye, uulize: Kulikoni? Jana mimi nilikwama, nikasema nimwambiye, hanong'ona sikioni Akasema: Don't murmur, hasema: Mama nnaye, sijui wateka nini! Kimombo tulokikopa, kina sisi chatuuma, chatukutisha madhila Kisa hiki ningakupa, japokuwa chanitoma, kina funzo la sahala Sima twali twaichapa, akaingia Fatuma, akatuona tukila Akanita: Juma's papa, hamba: Papa si wa Juma, lakini waweza kula Mohamed Khamis. Takaungu, Kenya 12.6.2022 |