ETIMOLOJIA YA NENO 'MAHARI' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'MAHARI' (/showthread.php?tid=2586) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'MAHARI' - MwlMaeda - 06-02-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'MAHARI' Neno *mahari* katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: ya-/ya-]* yenye maana ya mali anayotoa mwanamume na kuwapa wazazi wa mwanamke anayetarajia kumwoa; mali au fedha itolewayo na wazazi wa mwanamume kwa wazazi wa msichana anayetaka kuolewa. Neno *mahari* limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu *mahrun/mahran/mahrin مهر* lenye maana kile anachotoa mume kumpa mkewe kwa ajili ya kufunga ndoa kati yao. Neno lingine la Kiarabu lenye maana ya mahari ni *swadaaqu صداق.* Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu *mahrun مهر* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *mahari* maana yake katika lugha asili - Kiarabu haikubadilika. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |