MAJINA YA KIPARE NA MAANA ZAKE - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Historia ya makabila ya kibantu (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=15) +--- Thread: MAJINA YA KIPARE NA MAANA ZAKE (/showthread.php?tid=257) |
MAJINA YA KIPARE NA MAANA ZAKE - MwlMaeda - 06-24-2021 Wapare kama walivyo Wanyakyusa hutumia majina yenye maana mbalimbali na kwa kiasi kikubwa huwa yanamrejelea Mungu. Baadhi ya majina hayo ni:
1. ELIETI – MUNGU ANASEMA
2. ELIETINIZE – MUNGU ANASEMA NIJE
3. ELITWAZA – MUNGU TUMEKUJA
4. ELINAZA – MUNGU NIMEKUJA
5. ELITUWAHA – MUNGU TUKO HAPA
6. ELIMVONEIA – MUNGU NIHURUMIE
7. ELIENIGHENJA – MUNGU ANANISAIDIA
8. ELIENITUJA – MUNGU AMENIFARIJI
9. ELIATULIZA – MUNGU ANATULIZA
10. ELINAFIKA – MUNGU NIMEFIKA
11. ELIESIKIA – MUNGU ANASIKI/ANATUJALI
12. NAMINAZI/ZA – NAMI NIMEKUJA
13. NAGHENJWA – NIMESAIDIWA
14. NAMKUNDA – NIMEMPENDA (MUNGU)
15. TWAZIHIRWA – TUMEFURAHI
16. NIARIRA – NATARAJIA
17. NIMZIHIRWA – NAMFURAHIA (MUNGU)
18. NIGHENJIJWA – NILISAIDIWA (NA MUNGU)
19. NIMGURAELI – NAMSHIKA MUNGU
20. GURACHEDI – SHIKA CHEMA
21. NAVONEIWA – NIMEHURUMIWA
22. NIMSEMBA – NAMBEMBELEZA (MUNGU)
23. NIVONEIA – NIHURUMIE
24. NIMUINDAELI – NAMSUBIRI MUNGU
25. NAZAHEDI – NIMEKUJA PAZURI
26. TWAMZIA – TUMEMJIA (MUNGU)
27. KUNDAELI – MPENDE MUNGU
28. NARISHWA – NACHUNGWA (NA MUNGU)
29. NARISHWAHEDI – NACHUNGWA PAZURI
30. NAANJELA – NAABUDU
31. NIMUINDAELI – NAMSUBIRI MUNGU
32. NAFIKAHEDI – NIMEFIKA PAZURI
33. MBONEA – HURUMA
34. YONAZA – LEO NIMEKUJA
35. NAMSHITU – MSITU (Linahusishwa na msitu)
Yapo majina ya kipare yenye kuashiria misimu mbalimbali ya majira ya mwaka kama vile:
36. NAVURI – (Aliyezaliwa msimu wa vuli)
37. NAISHIKA – (Alizaliwa masika)
38. NAMBUA – (Alizaliwa msimu wa mvua, kwa mwanamke)
39. SEMBUA – (Alizaliwa kipindi cha mvua, mwanaume)
40. NAMSI – (Alizaliwa mchana)
41. NAKIO – (Alizaliwa usiku)
42. NANZA – (Alizaliwa kipindi cha njaa)
Wapare pia hutumia majina ya wanyama kama walivyo Wangoni ingawa majina yao hayako wazi kama ya Wangoni. mf
43. NANKUKU – KUKU
44. MTHETHE – MTETEA
45. NGUVE – NGURUWE
46. MASHUVE – MANYANI
47. KADEGHE – KINDEGE
48. KAGOSWE – KAPANYA
49. NKURUVI – JOGOO
50. KATHUNI – KASWALA
|