SHAIRI: POLE YAKO MAKANYILA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: POLE YAKO MAKANYILA (/showthread.php?tid=2542) |
SHAIRI: POLE YAKO MAKANYILA - MwlMaeda - 05-05-2022 POLE YAKO MAKANYILA Usifurahi mwanzoni, kauli huikumbuki? Yule mtunga diwani, alisema kitu hiki, Sasa umekuwa nyani, umezua taharuki, Idd tumekula sisi, pole yako Makanyila. Kutunga nimekawia, kwa shibe sitamaniki, Juzi ulisimulia, una wengi marafiki, Sifuri umeambua, na nyumbani hubanduki, Idd tumekula sisi, pole yako Makanyila. Yalizidi maakuli, jambo hili liafiki, Tukajaziwa bakuli, pilau nyama na siki, Na ule mweupe wali, ukaliwa kwa samaki, Idd tumekula sisi, pole yako Makanyila. Wale wapenda mtindi, hawakukosa wanzuki, Tulikesha kama bundi, hadi mida ya mswaki, Watu vikundi vikundi, tukaisahau dhiki, Idd tumekula sisi, pole yako Makanyila. Mdomo waacha wazi, kwa hili unahamaki, Wajawe wanakuhizi, vile unavyojinaki, Na ujuwe siku hizi, marafiki wazandiki, Idd tumekula sisi, pole yako Makanyila. Sasa wakuna sharubu, kimepita kitu hiki, Imekufika taabu, hakuna wakukulaki, Njaa ilikuadhibu, na kwako vile hupiki, Idd tumekula sisi, pole yako Makanyila. Kijiko umenunua, ukiwa mwenye mithaki, Kesho wenda kujilia, kula kwako hukumbuki, Mee! sasa unalia, umenuna haucheki, Idd tumekula sisi, pole yako Makanyila. Lifika kukusalimu, na hapa kwako sibaki, Ilivyonifika hamu, viporo vilivyobaki, Nikale mbuzi kwa ndimu, na leo kwangu sipiki, Idd tumekula sisi, pole yako Makanyila. Mtunzi Filieda Sanga Mama B Mabibo Dsm 0753738704 |