SHAIRI: KEMEENI VIGOMA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: KEMEENI VIGOMA (/showthread.php?tid=2512) |
SHAIRI: KEMEENI VIGOMA - MwlMaeda - 04-15-2022 KEMEENI VIGOMA Ngoma hizi mchezazo, hali wazi maungoni, Zinaleta angamizo, mnadhani hatuoni? Basi zitiwe katazo, hivi mwatufunza nini? Vikemeeni vigoma. Kina mama hususani, lawama nawangushia, Nauliza mwafanyani, ngomani mkisogea? Kujitia fedhehani, nasi tukiangalia, Hivi twajifunza nini? Enyi wapiga vigoma, kina baba maarufu, Sikieni ninasema, acheni huo uchafu, Mnatutia kilema, tusiwe waadilifu, Acheni hiyo tabia! Serikali Mtukufu, uliye chombo imara, Ondoeni usumbufu, maadili wanopora, Taifa hulikashifu, adabu ikose dira, Kamateni wachezaji. Wachezavyo ni hatari, sikia habari hizi, Vyote viungo vya Siri, twaviona siku hizi, Hata nyie mtakiri, walikofika walezi, Sheria zichukuliwe. Yanatufika madhila, watoto tutazameni, Tunalala bila kula, walezi wapo ngomani, Ndoani amani Wala, tunabaki madharani, Watoto tunateseka. Taona barabarani, wameunda misafara, Watoto nao njiani, hujiunga misafara, Hivi wanapata nini, kiongezacho fikira? Washitakini Wazazi. Mtunzi Filieda Sanga Mama B Mabibo Dsm 0753738704 |