SHAIRI: ROBO FAINALI CAF: NI SIMBA YA TANZANIA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: ROBO FAINALI CAF: NI SIMBA YA TANZANIA (/showthread.php?tid=2497) |
SHAIRI: ROBO FAINALI CAF: NI SIMBA YA TANZANIA - MwlMaeda - 04-04-2022 *ROBO FAINALI CAF: NI SIMBA YA TANZANIA* Ni usiku saa nne, Huu ni mwezi wa nne, Tumefunga goli nne, Simba Robo Fainali. Ndege tutazidi panda, Jinsi tunazidi shinda, Hata dau linapanda, Simba Robo Fainali. Wachezaji hongereni, Na makocha hongereni, Viongozi pongezini, Simba Robo Fainali. Katika ukanda huu, Simba ndiyo timu kuu, Katika mpira huu, Hiyo Robo Fainali. Siyo Kombe la Azam, Hiyo pokea salam, Huko kwa wataalam, Simba Robo Fainali. Lingekuwa goli moja, Wangeinuka pamoja, Sasa waishiwa hoja, Simba Robo Fainali. Wamepigwa Form Foo, Magoli manne goo, Na wenyeji wao loo, Simba Robo Fainali. Walikuwepo wachawi, Wakidhania hayawi, Wameshapakazwa kiwi, Simba Robo Fainali. Kesho itisha presi, Wandugu wenye mikosi, Hii foo jii kasi, Simba Robo Fainali. Amsha amsha yetu, Tunalala roho kwatu, Acha wenye roho butu, Simba Robo Fainali. Simba tunaisifia, Heshima kwa Tanzania, Hapo ilipofikia, Hiyo zaidi ya dili. Tembelea Tanzania, Vile watutangazia, Wengi wataangalia, Huko Robo Fainali. Watalii wakifika, Uchumi ukajengeka, Sote tunafaidika, Simba Robo Fainali. Ni Simba ya Tanzania, Robo imeshaingia, Heri tunaitakia, Izidishe kwenda mbali. Robo fainali CAF, Simba timu maarufu, Ni mpira maradufu, Chaenea Kiswahili. Na Lwaga Mwambande (KiMPAB) lwagha@gmail.com 0767223602 |