SHAIRI: MWENDANI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: MWENDANI (/showthread.php?tid=2418) |
SHAIRI: MWENDANI - MwlMaeda - 03-02-2022 MWENDANI 1. Mwendani wako mwendani, ukitaka umjuwe Ngia naye safarini, mwenende mwendo wa kuwe Au muate nyumbani, ukatembee ukawe Akosapo kuwa mwewe, huyo ni wako mwendani 2. Mwendani wako mwendani, ukitaka mjuato Mpishe ndia zenye mwani, zenye miba na tototo Au mbwagie zani, ambayo kwamba ni nzito Akuonyapo mapito, huyo ni wako mwendani 3. Mwendani wako mwendani, ukitaka mfeeli Moyowo utie kani, utumie yakwe mali Umuonapo haneni, hakuregeza kauli Hashabihi hamithili, huyo ni wako mwendani - Muyaka bin Haji (mshairi wa Mombasa, aliyeishi baina ya mwaka 1776 na 1840). *mwenende- mwende *mwendo wa kuwe - mwendo mrefu; masafa marefu *muate - mwache *ukawe - uchelewe *akosapo kuwa mwewe - asipokunyakulia/asipokuibia chako *ukitaka mjuato - ukitaka kumjua vizuri *mpishe ndia - mpitishe njia *tototo - tope *mbwagie zani - mwangushie balaa; mpe tatizo kubwa *akuonyapo mapito - akikuonesha njia za kupita (ili kutoka kwenye tatizo hilo) *ukitaka mfeeli - ukitaka kumtenda/kumjaribu *moyowo - moyo wako *hakuregeza kauli - hakusema neno; hakulalamika *hashabihi hamithili - hakutoa hata ishara ya kulalamika au kukasirika |