ETIMOLOJIA YA NENO 'AKISAMI' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'AKISAMI' (/showthread.php?tid=2409) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'AKISAMI' - MwlMaeda - 02-26-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AKISAMI' Neno *akisami* katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* yenye maana zifuatazo: 1. Sehemu ya kitu, umbo au tarakimu kama vile robo (1/4), theluthi (1/3), au nusu (1/2). 2. Umbo au namba isiyo kamili. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *aksami*( *soma: aqsaamun/aqsaaman/aqsaamin اقسام)* ni nomino ya Kiarabu, wingi wa neno la Kiarabu *qismun قسم* lenye maana ya fungu au sehemu ya kitu kilichogawanywa. Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu *aqsaamun/aqsaaman/aqsaamin أقسام)* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *aksami* maana yake katika lugha ya asili - Kiarabu haikubadilika. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |