MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'AKIDU' - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
ETIMOLOJIA YA NENO 'AKIDU' - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16)
+--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'AKIDU' (/showthread.php?tid=2406)

ETIMOLOJIA YA NENO 'AKIDU' - MwlMaeda - 02-21-2022

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AKIDU'

Neno *akidu* katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: a-/wa- wingi: maakidu]* yenye maana ya mtu anayefanya kazi kwa makubaliano ya kimkataba; mfanyakazi wa mkataba.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *akidu*( *soma: aaqidun/aaqidan/aaqidin عاقد )*  ni nomino ya Kiarabu - jina la mtendaji wa kitenzi cha Kiarabu *aqada عقد* chenye maana ya: (i) amefunga mfano kamba au fundo (ii) ameingia katika makubaliano fulani.(iii) amedhamini (iv) amefanya mahesabu. (v) ameyafunga maua pamoja. (vi) amemkwamisha mtu mwengine kwa kumuuliza maswali magumu. (vii) ameghadhibika na kuwa tayari kwa shari yoyote. (viii) amemkalifisha mwengine majukumu fulani.

Kinachodhihiri ni kuwa neno *aaqidun/aaqidan/aaqidin عقد* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *akidu* lilichukua kutoka katika lugha ya asili - Kiarabu maana moja ya mtu aliyeingia mkataba na ukahusishwa mkataka huo na kufanya kazi kwa malipo maalumu ilhali kwa Waarabu neno *aaqidun عاقد* katika lugha ya Kiarabu lina maana nyingi.   

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*