Pendo lidumisheni - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: Pendo lidumisheni (/showthread.php?tid=2400) |
Pendo lidumisheni - John John - 02-15-2022 PENDO LIDUMISHENI MTUNZI: JOHN L. JOHN Mwenzenu nawatafuta, utungo niwaghanie, Kuna mambo nimepata, nataka niwaambie, Pendo lenu dumisheni, lisitiwe walakini. Kwanza, Mola muombeni, yeye ndiye kimbilio, Awajalie amani, kila iitwapo leo, Pendo lenu adumishe, lisitiwe walakini. Pili, msiwe wepesi, yasemwayo kuamini, Upeni muda nafasi, ukweli kuubaini, Pendo lenu dumisheni, lisitiwe walakini. Tatu, shirikianeni, kwani umoja ni nguvu, Utengano kataeni, hata kama kwa mabavu, Pendo lenu dumisheni, lisitiwe walakini. Nne, vumilianeni, hasa nyakati za shida, Zenye nyingi tafurani, zisokuwa kawaida, Pendo lenu dumisheni, lisitiwe walakini. Mti ulio na tunda, ni sawa na lenu pendo, Wapo watu huliwinda, lianguke kwa kishindo, Pendo lenu dumisheni, lisitiwe walakini. Mtunzi: JOHN LUKAS JOHN 0788514751/0747225775 Baruapepe: jjohnlukas0788@gmail.com |