ETIMOLOJIA YA NENO 'AHARISHAURI' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'AHARISHAURI' (/showthread.php?tid=2256) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'AHARISHAURI' - MwlMaeda - 01-19-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AHARISHAURI' Neno aharishauri katika lugha ya Kiswahili ni nomino: [Ngeli: a-/-wa] yenye maana ya kundi la wanachama wenye malengo maalumu; wajumbe. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili aharishauri( soma: ahlush - shuraa اهل الشورى ) ni nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo: 1. Watu waliopewa mamlaka na madaraka ya kushauriana na kukata shauri/kupitisha uamuzi. 2. Neno shuraa likitanguliwa na neno majlis , hubeba maana ya baraza la ushauri ; bunge majlisush shuraa مجلس الشورى. 3. Jambo la kushauriana. Kinachodhihiri ni kuwa neno hili ahlush shuraa/shawri lilipoingia katika Kiswahili lilibadilika kuwa aharishauri na kuchukua maana mpya ya kundi la wanachama wenye malengo maalumu; wakumbe. Shukran sana. Khamis S.M. Mataka. |