SHAIRI: MFAUME - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: MFAUME (/showthread.php?tid=2159) |
SHAIRI: MFAUME - MwlMaeda - 01-12-2022 MFAUME vya kale ndio dhahabu, hebu kuwa mchunguzi, Imekushuka ghadhabu, kakupiku kwa ujuzi, Langu donda hunitibu, kwa sirinja na mizizi, Chambo yako sikuila, na babu yako ninae. Kijana uache gumu, huiwezi hii kazi, Wawezaje kunitibu, unashindia viazi? Mwishowe unipe tabu, iwe kazi huiwezi, Chambo yako sikuila, na babu yako ninae. Shairi ninakujibu, Mfaume nenda kozi, Siku ulipojaribu, nikabaini huwezi, Nenda kashike Kitabu, walimu wakupe kwizi, Chambo yako sikuila, na babu yako ninae. Nikwambe yalo nisibu, kuwa na huyu lazizi, Naamini utatubu, akusamehe Mwenyezi, Anajua huyu babu, Kama katoka Shirazi, Chambo yako sikuila, na babu yako ninae. Tena ushike adabu, mepata wapi makuzi? Babu ana maajabu, mweledi wa upembuzi, Jambo unalojaribu, taambua kikohozi, Chambo yako sikuila, na babu yako ninae. Ukimuona shaibu, kwa penzi hana ajizi, Wewe tastaajabu, mfano sikuelezi, Mapenzi ni mahesabu, uyajue matatuzi, Chambo yako sikuila, na babu yako ninae. Kijana unaharibu, na ujue sikuwazi, Unajitia aibu, hali huna utatuzi, Hauishiwi sababu, mithili yake mbaazi, Chambo yako sikuila, na babu yako ninae. Shairi ulipojibu, nilibaki bumbuwazi, Unamtania babu, kwenye kilo hakujazi, Yatakupata majibu, na mie simkatazi, Chambo yako sikuila, na babu yako ninae. Ninafunua Kitabu, zangu beti sikatizi, Nikushikishe adabu, uache wako utozi, Ona unapata tabu, ulivyoishiwa pozi, Chambo yako sikuila, na babu yako ninae. Mitindo ya Kiarabu, babu anipayo dozi, Wala sisumbui nibu, niitwe muongopezi, Mashine yake ajabu! Ni muhogo si kiazi, Chambo yako sikuila, na babu yako ninae. Na muda unanisibu, nende kwa babu mlezi, Sasa naifunga nibu, ukweli mekupa wazi, Umeyapata majibu, hoja na ufafanuzi, Chambo yako sikuila, na babu yako ninae. Mtunzi Filieda Sanga Mama B Mabibo Dsm 0753738704 |