NGONJERA: TIMIZA NDOTO ZAKO - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: NGONJERA: TIMIZA NDOTO ZAKO (/showthread.php?tid=2118) |
NGONJERA: TIMIZA NDOTO ZAKO - MwlMaeda - 01-11-2022 SARAH: Uwanjani naingia, salamu kuwa mwagia, Kwa mbwembwe nimewajia, kitu nataka wambia,
Kaa makini sikia, mbiu badili tabia,
Kaka dada badilika, utumizi ndoto zako.
JOHN: Ipende nafsi yako, jenga roho yako hofu,
Mpende huyo mwenzako, usimletee tifu,
Muweke upande wako, ajenge uaminifu,
Kaka dada badilika, utimize ndoto zako.
SARAH: Wapo walokosea sana, sasa wanajutia,
Uamuzi kuvamia, busara kutotumia,
Mara tu kuamua, anasa kuzivamia,
Kaka dada badilika, utimize ndoto zako.
ABDI: Tena njia ni rahisi, haihitaji mateso,
Wala sio kwa kisi, na wala sio mguzo,
Tusipende kujihisi, kupima tusione so,
Kaka dada badilika, utimize ndoto zako.
SARAH: Usiwe kiruka njia, shimoni utaingia,
Mmoja anakufaa, wengine wote achia,
Tena utajishindia, maisha kufurahia,
Kaka dada badilika, utimize ndoto zako.
ABDI: Mwenzako ukamtunza, ukamwonesha upendo,
Hata yeye ukamfunza, na yeye awe ni lindo,
Asijeleta mafunza, kama kuku mdondo,
Kaka dada badilika, utimize ndoto zako.
JERRY: Mwamini kwa kila hali, hata akiwa fukara,
Msifanye kwa ukali, wengine waone fara,
Usiwe ka pilipili, hata ukiwa chotara,
Kaka dada badilika, utimize ndoto zako.
PETER: Kuwa kijana hodari, wa kuzishinda hisia,
Epuka mambo hatari, marafiki waso faa,
Fanya kwa kutafakari, taji utajitwalia,
Kaka dada badilika,utimize ndoto zako.
LEILA: Nyuma usiangalie, mbele na mmoja songa,
Wengine wasikuchezee, ukafanya ujinga,
Zawadi umpelekee, umpendaye ndoa funga,
Kaka dada badilika, ndoto zako utimize.
SARAH: Hapa mwisho nimefika, uaminifu mzuri,
Na tena utasifika, kwa tabia yako nzuri,
Kazini kuwajibika, kujenga taifa zuri,
Kaka dada badilika, utimize ndoto zako. |