SHAIRI: USIONE UKADHANI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: USIONE UKADHANI (/showthread.php?tid=2114) |
SHAIRI: USIONE UKADHANI - MwlMaeda - 01-11-2022 Dunia rangi rangile, methali hii muhimu
Usione jambo lile, ukadhani la dawamu
Kila chombo na wimbile, hilo mwenzangu fahamu
Usione ukadhani
Usione mtu yule, hana maisha matamuUkamsonda kwa ndole, kama kaila haramu Aso hili ana lile, nakujuza muadhamu Usione ukadhani Ati kamaliza shule, ana vyeti kemkemu Aranda huku na kule,mithili mwenye wazimu Hawi wa hivyo milele, siku yake itatimu Usione ukadhani Usimuone na yule, juu ni yake sehemu Halipuuzwi nenole, hadhi yake maalumu Hadumu hivyo milele, mpanga mambo Karimu Usione ukadhani Usimwone mwenye ndwele, haponi ukakalimu Dhana hizo ziondole, kichwanimwo zisidumu Hwenda mzima afile, mwele akatabasamu Usione ukadhani Maisha tangia kale, kueleweka vigumu Yataka mwenye makele, kichwani alo timamu Ndipo kunga amanyile, kwa mambo anozuumu Usione ukadhani Tama hapa niketile, nashusha yangu kalamu Haya ndugu yashikile, upate mastakimu Ila kiyatupa kule,utachekesha kaumu Usione ukadhani |