SHAIRI: WANETU WAMEPOTEA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: WANETU WAMEPOTEA (/showthread.php?tid=2112) |
SHAIRI: WANETU WAMEPOTEA - MwlMaeda - 01-11-2022 WENETU WAMEPOTEA
Wamepotea wenetu, katika ile ajali, kulia ninathubutu, raha imekaa mbali, ni wadogo wanakwetu, wameenda kwa Jalali, msiba ulotufika, ni msiba wa taifa.
Vurugu zile za chama, kwanza zikae pembeni,
Tuziepushe lawama, kama zile za chamani,
Tumuombeni karima., roho ziende peponi
Maafa yalotufika, ni maafa ya taiga.
Wenetu liliwajaza, gari lile maluuni,
Mwishowe limetuliza, wazazi huku nyumbani,
Tunabaki tunawaza,Hii ni ajabu gani??
Msiba ulotufika, ni msiba wa taifa.
Pia lilikuwa bovu, mesikia karibuni
Enyi muwe wasikivu,Na niwahadithieni,
Lilijaa na ubovu,Lilitoka gerejini,
Ni msiba wa wenetu, kila mtaa kilio.
Kifo ni kifo jamani, cha wenetu kinauma, wenetu Hawa jamani, wamepoteza uzima, wamehama duniani, kwa mola wende SALAMA,
Msiba ni wetu site, tuwaombee kwa mungu.
Tunataka hatutaki, hakuna ataegoma,
Hayuko ataebaki,sisi na watu wazima, ni kuanzia samaki, binadamu na wanyama, tuwaombee wenetu, wende jannatu naima.
Kumbukumbu ya ajali ya wanafunzi wa shule ya Lucky ya Arusha iliyotokea Rhotia –Marera
|