SHAIRI: WALALE PEMA PEPONI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: WALALE PEMA PEPONI (/showthread.php?tid=2111) |
SHAIRI: WALALE PEMA PEPONI - MwlMaeda - 01-11-2022 WALALE PEMA PEPONI
Hautupoi uchungu, kila uchwao machozi
Pengine ndo letu fungu, Ela kwahili siwezi
Leo nasema na Mngu, Kwa hino tungo ya wazi
Tunakuomba Mwenyezi, walaze pema peponi
Vililo vimetawala, ambatano na majonzi
Ndimi nimeshindwa kula, vipi kwa wao wazazi
Sipingi yako jaala, Wewe hakimu azizi
Tunakuomba Mwenyezi walaze pema peponi
Kifo kingalichanguwa, tungakuomba mjuzi
Hawa waweze kukuwa, kisha wafanye na kazi
Wallahi kwa hili kuwa, machozi thama machozi
Tunakuomba Mwenyezi, walaze pema peponi
Twakuomba Rahmani, mwenye mema maamuzi
Moja kwa moja peponi, yakawe yao makazi
Uifanye ihsani, pia kwa wao wazazi
Tunakuomba Mwenyezi, walaze pema peponi
Mwili unatetemeka, kuendelea siwezi
Chozi lanichuruzika, lakufanya simaizi
Sikulaumu Rabuka, kwenye wako uteuzi
Tunakuomba Mwenyezi, walaze pema peponi
MBARUKU ALLY
MOTO WENU Jr
0717199835
06/05/2017
23:10
CHUO KIKUU DODOMA
TANZANIA
|