SHAIRI: NA NIKIFA WASICHANGE - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: NA NIKIFA WASICHANGE (/showthread.php?tid=2104) |
SHAIRI: NA NIKIFA WASICHANGE - MwlMaeda - 01-11-2022 NA NIKIFA WASICHANGE Ewe mwanangu taali, Njoo hapa kwenye mwanga Njoo usiketi mbali, Kisha na mlango funga Nataka kupa kauli, ishike kama usinga Nikifa wasijechanga, ishike hii kauli Ndiye wewe wa awali, rika si mwana mchanga Timamu zako akili, huna chembe ya ubunga Ninakupa uwakili, usikubali matanga Nikifa wasijechanga, ishike hii kauli Sinazo nguvu za mwili, kwa maradhi kunizonga Mwanangu wajidhalili, mikono kwao kukinga Hupati japo kalili, wote wakupiga chenga Nikifa wasijechanga, ishike hii kauli Leo ni dhoofu hali, ndiyo kisa wanitenga Niliwalea azali, maisha yao kujenga Sasa nipo muhimbili, Dawa za kuungaunga Nikifa wasijechanga, ishike hii kauli Huu ni mwaka wa pili, toka nipate majanga Moyo unatundu mbili, yangu moja imefunga Dhati nateseka kweli, wafumba yao maninga Nikifa wasijechanga, ishike hii kauli Daftari na bakuli, wakipitisha kuchanga Piga teke vyende mbali, usishiriki ujinga Nakuomba wakabili, usihofu zao ngenga Nikifa wasijechanga, ishike hii kauli Mauti yakiwasili, ombi nizikwe Mkinga Moa kijiji aali, sitaki kuzikwa Vanga Mwanangu wosia mali, wapuuzao hutanga Nikifa wasijechanga, ishike hii kauli Hapa natia kufuli, na hotuba kuifunga Wewe wangu abtali, tayari nishakuganga hima fanya kulihali, yangu usijeyatenga Nikifa wasijechanga, ishike hii kauli MBARUKU ALLY MOTO WENU Jr (FAHARI YA TANGA) |