MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI: AOZWE NANI ? (SWALI) - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
SHAIRI: AOZWE NANI ? (SWALI) - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6)
+---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50)
+---- Thread: SHAIRI: AOZWE NANI ? (SWALI) (/showthread.php?tid=2082)

SHAIRI: AOZWE NANI ? (SWALI) - MwlMaeda - 01-10-2022

AOZWE NANI ? (SWALI)
Swabalkheri walimu,mashekhe nanyi makadhi….
Nawajia maimamu,mnifae tilimidhi…
Nnalo swali adhwimu,nawaomba mniridhi….
Hivi ataozwa nani,peponi tukijaliwa!?
Walikua maharusi,ndoa wakatunza sana….
Mapenzi ya ufanisi,wawili walipendana….
Sio kwamba ni nuhusi,kwa kifo wakatengana…
Hivi ataozwa nani,peponi tukijaliwa!?
Akawa bibi mjane,kila siku yunalia….
Na usiku wa manane,hakuwacha muwazia….
Hikuwa wafarakane,ila amri ya Jalia….
Hivi ataozwa nani,peponi tukijaliwa!?
Akamuwekea eda,kwa mbeko na taadhima…
Mirathi ikawa ada,akagawiwa salama….
Hakuwa na la ziada,akajitenga kwa wema….
Hivi ataozwa nani,peponi tukijaliwa!?
Miaka ikakatika,akaja kuposwa tena…
Bibie akaoleka,na akampenda bwana…
Ndoa ikaimarika,kama awali kufana…
Hivi ataozwa nani,peponi tukijaliwa!?
Mume huyu pia kafa,eda tena akakaa…
Ilivyo hii sadifa,peke yake akakaa…
Akawa mja wa sifa,wa ibada pia twaa….
Hivi ataozwa nani,peponi tukijaliwa!?
Kwa rehema zake Mungu,wakawa ni wa peponi…
Walikua wacha Mungu,hawakufata shetwani…
Nijuzani nyi wenzangu,mke ataozwa ani….
Hivi ataozwa nani,peponi tukijaliwa!?
Nane ndo yangu tamati,nikisubiria jibu….
Ni Teja Alobahati,nalitafuta jawabu…
Niambani la thabiti,dawa ya swali kujibu….
Hivi atazwa nani,peponi tukijaliwa!?
(Ali Salim Masito)
NI MKE ATACHAGUA (JIBU)
Waaleykum salamu, nakamilisha faradhi
Mbaruku si imamu, wala sinao ukadhi
Ela imenilazimu, nitoe njema lafudhi
Ni mke atachagua, wa mwanzo au wa pili
Ni kweli wala si hisi, hayano ninayonena
Atapatiwa nafasi, peponi wakikutana
Na nani atajilisi, kati ya wale mabwana
Ni mke atachagua, wa mwanzo au wa pili
Hata wangali wanne, waume walotimia
Mke tauzwa anene, yupi alomridhia
Lengo maisha yafane, kwenye pepo ya Jalia
Ni mke atachagua, wa mwanzo au wa pili
Huko hakuna upweke, kwenye pepo ya Manani
Mkosa ‘tapewa mke, mzuri hurul’aini
Tena kwa chaguo lake, mwenye uzuri wa shani
Ila mke ‘tachagua, wa mwanzo au wa pili
Zako nane zangu tano, siongezi tena beti
Lipokee jibu nono, Teja ulo na bahati
Katu simalizi wino, nitajike na umati
Mbaruku sina neno, ni kiganjani kwa M’ngu
MBARUKU ALLY
 
MOTO WENU