SHAIRI: KIFO - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: KIFO (/showthread.php?tid=2081) |
SHAIRI: KIFO - MwlMaeda - 01-10-2022 KIFO Kifo kimekuwa siri, aijuwaye Mwenyezi Kaficha Mola Jabbari, hakutaka kiwe wazi, Huja pasipo habari, fumbo hili hatuwezi, Leo yule kesho mimi, kila nafsi itakufa. Kifo hakina fulani, kuchaguwa kama nazi, Alipangalo Manani, binadamu huliwezi, Wote wake ikhiwani, Muumbaji mwenye enzi, Leo yule kesho mimi, kila nafsi itakufa. Kifo kipo ujinini, hakinacho ubaguzi, Mbinguni na aridhini, atabakia Mwenyezi, Kaenda Suleimani, na Muhammad kipenzi, Leo yule kesho mimi, kila nafsi itakufa. Kifo huja kitandani, kiwa tele usingzi, Hakina habari gani, japo hili umaizi, Kifo hakijui nani, mjomba wala shangazi, Leo yule kesho mimi, kila nafsi itakufa. Kifo hujuwa Dayani, Mola aliye mlezi, Kichwa naye kaburini, msizione tungizi, Ati champata nini, hamtamwona mtunzi, Leo yule kesho mimi, kila nafsi itakufa. Kifo kipo kila nafsi, hukifichi kwa irizi, Chozi lanitoka Rasi, kuandika sikuwezi, Kaditama nisihasi, niliache simulizi, Leo yule kesho mimi, kila nafsi itakufa. Rasi Saidi Mbwana Kichwa cha Kale 0718286677 |