SHAIRI: WASIA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: WASIA (/showthread.php?tid=2080) |
SHAIRI: WASIA - MwlMaeda - 01-10-2022 WASIA Naapa kwa nyota tano, angani zinoelea Na kwa huu muagano, niuyako narejea Ushike wasia huno, ambao nakumegea Kifo chaninyemelea, yashike yangu maneno Kuno kunena kwa wino, mosi kinywa chalemea Yamepukutika meno, na fizi kunilegea Udenda kumwaga kuno, wema ‘siche nitendea Kifo chaninyemelea, yashike yangu maneno Ndoa ni maridhiano, huyuno ‘metuletea Ufakiri siyo neno, ata ungaselelea Usitembeze kiuno, viwavi kujiletea Kifo chaninyemelea, yashike yangu maneno Mazishi ya jumatano, juma lililopotea Kisa’che ndiyo mguno, mwenzio kujifyelea Sitaki wende hivino, waambe sijakulea Kifo chaninyemelea, yashike yangu maneno Chukua wangu mfano, nisiloona umbea Simcha wa malumbano, na ovyo kujisemea Madhila yakiwa mno, Mola namuelekea Kifo chaninyemelea, yashike yangu maneno Busara yake mavuno, wema ukuongezea Pamwe hekima vivino, amani ukuletea ‘Kiabudu mivutano, dhiki utaogelea Kifo chaninyemelea, yashike yangu maneno Ikiwa mfarakano, ndoani umetokea Yaepuke mapambano, lengo usirudi bea Samahani huwa chano, hasira zinapomea Kifo chaninyemelea, yashike yangu maneno Kutetemeka mkono, ambavyo wajionea Ni kwakuja kwake yuno, uhai ‘nojibebea Kutokwa roho ndo kuno?, sina cha kuongezea Kifo chaninyemelea, yashike yangu maneno MBARUKU ALLY MOTO WENU 0717199835 23/12/2017 |