SHAIRI: SINA NAFUU - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: SINA NAFUU (/showthread.php?tid=2077) |
SHAIRI: SINA NAFUU - MwlMaeda - 01-10-2022 SINA NAFUU Kula mie ninakula, bila kula sijilazi, Langu tatizo kulala, japo ni mema malazi, Najaribu Ila wala, siupati usingingizi, Yananitesa mapenzi, mwenzenu sina nafuu. Daima ninamuwaza, mwendani wangu lazizi, Vile ananipuuza, ninakonda siku hizi, Hata nikimueleza, hunita mie mpuzi, Yananitesa mapenzi, mwenzenu sina nafuu. Ashiki mwili mzima, kuhimili siiwezi, Jamani nisijezima, inikatike pumzi, Msione nalalama, hali yangu sijiwezi, Yananitesa mapenzi, mwenzenu sina nafuu. Usiku wa katikati, ninakesha kama mwizi, Nadhani sina bahati, au tatizo ujuzi, Moyo wangu hatihati, yanimwagika machozi, Yananitesa mapenzi, mwenzenu sina nafuu. Kiwa kuna matibabu, inifae hiyo dozi, Niondokewe taabu, niwe kama mwaka juzi, Leo yanayonibu, kusimulia siwezi, Yananitesa mapenzi, mwenzenu sina nafuu. Ninazidi kuteseka,vile sina muuguzi, Wengine wananicheka, eti mie siyawezi, Donda limenifumuka, maumivu hayapozi, Yananitesa mapenzi, mwenzenu sina nafuu. Kitu niwaambiacho, kilianzia miezi, |