MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'AFYUNI - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
ETIMOLOJIA YA NENO 'AFYUNI - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16)
+--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'AFYUNI (/showthread.php?tid=2051)

ETIMOLOJIA YA NENO 'AFYUNI - MwlMaeda - 01-07-2022

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AFYUNI'

Neno *afyuni* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino [Ngeli:i-/i-]* yenye maana ya 'kileo chenye umbo la kidonge kunachotengenezwa kutokana na utomvu wa *mpopi*( *afyuni* ) , ambacho kwa kawaida hutumika kama tiba ya kutuliza maumivu, aghalabu hutumiwa kinyume cha sheria kama dawa  ya kulevya.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *afyuni* (soma: *afyuunun/afyuunan/afyuunib افيون)* lina maana ya 'dutu inayotolewa kwenye mpopi (afyuni) ambayo inatia ganzi na hutumiwa kwa kutuliza maumivu na kuleta usingizi, pia hutumika vibaya kama dawa ya kulevya.

Kinachodhihiri ni kuwa neno *afyuni* ( *soma: afyuunun/afyuunan/afyuunin افيون*) lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa  kuwa neno *afyuni* halikubadili maana yake ya msingi katika  lugha ya asili - Kiarabu.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*