SHAIRI: MGANGA NI MUNGU - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: MGANGA NI MUNGU (/showthread.php?tid=2041) |
SHAIRI: MGANGA NI MUNGU - MwlMaeda - 01-06-2022 MGANGA NI M’NGU Shairi nalitungile, lije kwenu walimwengu Ndanimwe lina makele, lisomeni ndugu zangu Si fumbo lende kwa yule, usiku mvunja vyungu Mganga wangu ni M’ngu, Nawambia msikile Nawambia msikile, mganga wangu ni M’ngu Ndo kisa ile mishale, katu haifiki kwangu Kila chombo na wimbile, msemo wa kaka yangu Anilindaye Mlungu, si hirizi nawambile Si hirizi nawambile, anilindaye Mlungu Kwake mwilini zi tele, kesha mafungu mafungu Paka mia achinjile, hafiki daraja langu Mkombozi wangu Mungu, hawezi kunipa ndwele Hawezi kunipa ndwele, mkombozi wangu Mungu Vilingeni ashindile, haishiki nyota yangu Sijida kwa muumbile, wa ardhi nayo mbingu Akiabudu mizungu, atakuja afilile Atakuja afilile, akiabudu mizungu Tamati natamatile, mwambieni Mlimwengu Mimi ni mja vivile, ana yake nina yangu Riziki ilo ya kwangu, sihiri aishikile MBARUKU ALLY MOTO WENU 0717199835 Nikiwa Dodoma Mzaliwa Moa Tanga |