SHAIRI: JOYA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: JOYA (/showthread.php?tid=2038) |
SHAIRI: JOYA - MwlMaeda - 01-06-2022 >>> JOYA <<<<. Nazi niliyonunua, nimekuta joya ndani. Ndipo nikafurahia, kuila kwa umakini. Baada kujibwagia,ladha yake sitamani Joya lina ladha gani, malenga niambiyeni ? Ukitazama kwa macho, nyeupe nyama laini. Huliwa kwake kificho, mja hali hadharani. Malenga ni chambilicho, majoya hayalingani. Joya lina ladha gani, malenga niambiyeni? Wapendayo husifia, raha iko utosini. Wao wanapojilia, husema tamu ayuni. Kwangu naona fadhaa, kulila silitamani. Joya lina ladha gani, malenga niyambiyeni. Hebu nasi tuambie, utamu wa joya nini. Nazi tena ninunue, nile joya ukumbini. Nambie nami nijue, isiwe ni kutuhini. Joya lina ladha gani, malenga tuambiyeni? Beti zangu nii haba, nakomea kituoni. Akina mama na baba, joya lina kitu gani. Wengj hula wakishiba, joya lina siri gani. Joya lina siri gani, na ladha tuambiyeni. WAHENGA NAOMBENI JIBU AMOUR joya
NOMINO
Matamshi
joya/ʄɔja/ |