MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI : MOLA WAPE WANIPAO (1) - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
SHAIRI : MOLA WAPE WANIPAO (1) - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6)
+---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50)
+---- Thread: SHAIRI : MOLA WAPE WANIPAO (1) (/showthread.php?tid=2032)

SHAIRI : MOLA WAPE WANIPAO (1) - MwlMaeda - 01-06-2022

Umenigusa mtima, kwa hicho chako kiliyo
Nami moyo waniuma, nikitazama haliyo
Ndipo utungo nafuma, usihisi u pekeyo
Usiupe dhiki moyo, ya duniani hukoma
Heko kwako na heshima, awali kwa imaniyo
Humkufuru Karima, kwa yote yakusibuyo
Kuyakabili nasema, hakika yataka moyo
Sijidhiki mno moyo, duniani si daima
Pongezi zangu natuma, kwa auni wakupao
Ni wema wa juu kima, si wengi tuuwezao
Ila wao wajituma, mawio hata machweo
Usiupe dhiki moyo, Mwenyezi anakupima
Shukuru haswa neema, kuruzukiwa mkeo
Shukuru hilo daima, kujaliwa kama huyo
Hiyo neema adhima, wengi mno wasonayo
Sijidhiki mno moyo, taraji hatima njema
Ingawa kweli yauma, tambua ni yapitayo
Ya dunia si daima, raha na yaumizayo
Huzunini sije zama, Mbaruku kaza moyo
Usiupe dhiki moyo, thawabu juwa wachuma
Imara yakhe simama, ushinde yakupatayo
Yasikupige mtama, ukakosa farajayo
Hiyo siku ya kiama, malipo ya subirayo
Sijidhiki mno moyo, sikae washika tama
Kumbuka bishara njema, kwa waja wasubiriyo
Mwenye subira huchuma, mavuno atamaniyo
Subira njema daima, situpe funguo hiyo
Usiupe dhiki moyo, saburi ndugu andama
Tumia vyema uzima, kwa ibada uwezayo
Atakujaza Rahima, lokupa mitihaniyo
Sote twombe mwisho mwema, siri ya Mola yajayo
Sijidhiki mno moyo, Mola mwingi wa huruma
Kuhitimisha nudhuma, ninatoa zingatio
Tungali wanaadama, twaumbwa tupumuwao
Mgonjwa au mzima, mwiko kucheka mwenzio
Usiupe dhiki moyo, tudhibiti tunosema
Ni mimi nisiyevuma, wachache wanijuwao
Lilengane nilofuma, utungo uusomao
Nainuka kaditama, ninakifunga kikao
Sijidhiki mno moyo, Mndenge ninasimama
(LILITUNGWA NA ALHAJ OSAN OMARI NGULANGWA 10/04/2016)