MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI : BARUA KWA WASHAIRI - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
SHAIRI : BARUA KWA WASHAIRI - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6)
+---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50)
+---- Thread: SHAIRI : BARUA KWA WASHAIRI (/showthread.php?tid=2021)

SHAIRI : BARUA KWA WASHAIRI - MwlMaeda - 01-05-2022

Barua kwa washairi, Mbaruku naandika
Kwa haya yanodhihiri, kusubiri sijataka
Kheri iwe nusu shari, siyo ya kukamilika
Na tusipobadilika, twajichimbia kaburi
Wavyele wanalaani, vikali yanotendeka
Waniuza kulikoni, mbona kamba yakatika?
M’nambe niwambe nini, neno moja la hakika
Ndia tuliyoishika, twajichimbia kaburi
Nimeona chozi lake, Jimbi Muhaji Muyaka
Anarusha na mateke, dhati anasikitika
Matendoye tuyashike, nasi tujekutajika
Yake tusipo yashika, twajichimbia kaburi
Punde Shabani Robati, kichwa chini kaibuka
Kanipa tenzi ya Hati, na ya Adili sadaka
Wa washairi umati, tusome hizi haraka
Tenzize kuziepuka, twajichimbia kaburi

Hapo tena sikulala, jasho lanitiririka
Akaja Mnyampala, kwa hasira anafoka
Kasema tuwache hila, hila ni mbaya huluka
Hila zikidhihirika, twajichimbia kaburi
‘Kashikwa na Jinamizi, Zakuwany msifika
Nikapatwa bumbuwazi, yale aliotamka
Tukate kwanza mizizi, fitina itaondoka
Fitina kuieleka, twajichimbia kaburi
Nikapokea bakora, sijui wapi zatoka
Kumbe ni mwalimu Pera, chozi lam’bubujika
Tusiabudu idhara, yetu nnje kuanika
Hapano tulipofika, twajichimbia kaburi
Mwisho akapiga simu, mbio nikenda ishika
Jitukali muadhwamu, mema akayaanika
Kanamba shika kalamu, sema ya kuweleweka
Hekima tukizizika, twajichimbia kaburi
Washairi pulikani, tutende ya kuongoka
Vita tuviepukeni, matunda yake mashaka
Mimi ninakwambieni, wazee waloyataka
Kutwaa hila ya nyoka, twajichimbia kaburi
Kwa heri ya kuonana, narudi nilipotoka
Washairi huzikana, si leo toka miaka
Kwa haya ninayoona, tutauwana kwa shoka
Haya tusipokumbuka, twajichimbia kaburi
MBARUKU ALLY
MOTO WENU
0717199835
22/01/2018