SHAIRI : YAZAMISHE BAHARINI MAKOSA YA MKE WAKO - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI : YAZAMISHE BAHARINI MAKOSA YA MKE WAKO (/showthread.php?tid=2013) |
SHAIRI : YAZAMISHE BAHARINI MAKOSA YA MKE WAKO - MwlMaeda - 01-04-2022 Kwa mapana nakusifu hakika metakasika mola wangu mtukufu Wa majini malaika Fadhila zako kunjufu kila pahala zafika Kwa baba wa familia Zifike zangu salamu Kwenye maisha ya ndoa Changamoto na matamu Mkeo anakosea Hakuumbwa maasumu yazamishe baharini Makosa ya mke wako Ishi nae kwa makini Huyo ni ubavu wako simjeruhi usoni Kumpiga iwe mwiko Ni bahari ya mapenzi yenye maji kila kona Makosa ya kipuuzi Jifanye hujayaona Mpe bora ya malezi Ajisikie mwanana Usijitie ujeshi Ati wampa adabu Na makosa hayaishi Kuwa mume si sababu Ukiwa kwao mcheshi Kwako mwanaume gubu Madhali sio haramu Vikosa vya kawaida Mpe maneno matamu Azidi pata faida Maneno haya fahamu Hukumuoa kwa shida Ebwane mke hapigwi kwa bakora za mitini Anapigwa kwa mahaba Yalozama baharini Mzamishe habahaba Hadi aloe mwilini Ukihisi Anajuta Kwa alichokufanyia Mpe mabusu matata Huku Ukimsifia Mwambie”kwako nadata” “Wala hujanikosea” Mletee vizawadi nyumbani ukirejea Kuwa mume maridadi Epuka kumkemea Atakupenda zaidi Haya Ukizingatia Akikosea kupika Tena isiwe kasheshe jitahidi kuridhika Chakula chake ukishe Maneno haya hakika Jaribu uhakikishe Mkeo akikuudhi Usivunje wake utu utajitia maradhi kukosoa kila kitu Onyesha umemridhi kununa usithubutu Akiichupa mipaka Ya haramu kuyafanya Hapo hapana mashaka Ni lazima kumuonya Katu sifanye dhihaka Ni wajibu kumkanya Akikudai talaka Nakusihi simjibu Ni hasira kwa hakika zitapoa taratibu Ukipaniki haraka ataenda pata tabu Ataolewa na nani? Ukishamuacha wewe? Aolewe na muhuni? atajijua mwenyewe? Na weye taoa jini? Hakosei kama wewe? Ukingoni nimegota Naomba kuwasilisha Kwa pale nilipopata Mola kaniwafikisha Yarabi tupe thabata Na ndoa kuzidumisha… Mtunzi: Al akh Abuu hafsa |