SHAIRI : AKIMBIA PAFIWAKO ENDA WALIWAKO NYAMA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI : AKIMBIA PAFIWAKO ENDA WALIWAKO NYAMA (/showthread.php?tid=2012) |
SHAIRI : AKIMBIA PAFIWAKO ENDA WALIWAKO NYAMA - MwlMaeda - 01-04-2022 Nimeshamsabiliya, sina nongwa wala ngowa
‘Ngawa ‘mepoteya njiya, kisha kujitia dowa
Huruma namuoneya, heshimaye kujivuwa
Nguo ameshajivuwa, kacheza pata poteya
Nguo ameshajivuwa, kacheza pata poteya
Rabbi haya wayajuwa, ingawa nakuambiya
Mola utakalo huwa, basi nami nitendeya
Kakimbiya pafiwako, na alipoelekea
Akimbiya pafiwako, na alipoelekeya
Ndipo nyama waliwako, baada ya kujifiya
Na aselelee huko, asijepo nirudiya
Kwa aliyonitendeya, kiliyo changu ki kwako
Kwa aliyonitendeya, kiliyo changu ki kwako
Rabbi mdhihirishiya, yote yaliyoko huko
Apate kujioneya, nami nipate kicheko
Mola yafanye mapema, kabula yangu mauko
Mola yafanye mapema, kabula yangu mauko
Ujue umma mzima, wote wa hapa tuliko
Ili nibaki salama, niondoe sikitiko
Mwisho wa langu andiko, Mbaruku nasimama
MBARUKU ALLY
MOTO WENU
0717199835
Mzaliwa Moa Tanga
|