MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI : SILIPIZI - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
SHAIRI : SILIPIZI - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6)
+---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50)
+---- Thread: SHAIRI : SILIPIZI (/showthread.php?tid=2010)

SHAIRI : SILIPIZI - MwlMaeda - 01-04-2022

SILIPIZI
Nduu nakujuza, umaizi
Ngoma unocheza, ipo wazi
‘Ngawa nayaweza, silipizi

Wapita tangaza, kwa majazi
Hujaniangaza, mpuuzi
Mnipa mwangaza, ni Mwenyezi

Yananiumiza, maenezi
Kesha yaniliza, sinyamazi
Nilinde Muweza, sijiwezi

Nyuma kugeuza, siyo kazi
Ela najikaza, sigeuzi
Unajipoteza, m’bazazi

Hapa nasooza, siongezi
Ninakueleza, wazi wazi
Yako kulipiza, si tatizi

MBARUKU ALLY
MOTO WENU
0717199835