SHAIRI : KUAMBIANA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI : KUAMBIANA (/showthread.php?tid=2009) |
SHAIRI : KUAMBIANA - MwlMaeda - 01-04-2022 ?SHAIRI : KUAMBIANA? Panga lilokata shina, kukata tawi katiti Usivimbe na kutuna, kwa kuwekwa juu ya mti Mpanga yote Rabana, usinajisi bahati Waziviza zako hati, kulumba yaso maana Kiburi si maungwana, hapa nazikaza nati Nasema niloyaona, sisemi ya hatihati Aliye hai mchana, usiku ndiye maiti Nanena nao umati, nami mumo pasi kona Vikombe vinagongana, viwapo kwenye kabati Nakuambiya bayana, na vi tele vizibiti Lililo m’bwaga jana, mgema ni lile kuti Ola chako kizingiti, na mazoea achana Pokea yangu semina, usinilipe senti Ni ada kukumbushana, katika hizi nyakati Nataka tujezikana, sisi wa moja baiti Endeleza harakati, ulitunze lako jina Kwa kheri ya kuonana, naivua helmeti Tambua utu hazina, na matendo hasanati Na changi kuchangizana, njoo tukutane kati Usinipige manati, siyo vyema kugombana MBARUKU ALLY MOTO WENU 0717199835 |