SHAIRI : SINENI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI : SINENI (/showthread.php?tid=2008) |
SHAIRI : SINENI - MwlMaeda - 01-04-2022 Sineni mwana kunena,sitamki nilonayo.
Ndani yalo fichamana,moyo yaniunguzayo.
sitoyaweka bayana,mazito yanisibuyo.
Sineni katu sineni,siwi kama wanenao.
ngaumwa ndani kwa ndani,simanzi kila uchao.
tasalia subirani,hadi siku ya pumbao.
Sineni na sisubutu,daima sisimulii.
sibainishi kwa watu,kwa vyovyote siwambii.
kwao sitaraji kitu,bora kunyamaza zii.
Sineni nineneeni,matozi yanimwagike.
nijitie mawazoni,bilashi nihuzunike.
ninganena ifaeni,jeraha litonesheke.
Sineni hapa ni mwisho,sitokwenda mbali mno.
sitowatwika uchosho,nikazua minong’ono.
sitowatoa na jasho,zinatosha beti tano.
KIBWAGIZO.
siyaweki hadharani,tasubiri mwisho wake.
SARAI MAULIDI
MOMBASA,KENYA.
|