MFANO WA MAJIGAMBO - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: MFANO WA MAJIGAMBO (/showthread.php?tid=1988) |
MFANO WA MAJIGAMBO - MwlMaeda - 01-04-2022 MFANO WA MAJIGAMBO
Mimi ni nani? Mimi ni fulani bin fulani
Mimi ndiye niliyemkomesha yule mshenzi
Yule samba kasoro mkia!
Mimi ndiye yule ninayepigana kifua wazi
Ilinichukua muda mfupi tu kumkomesha!
Kumkomesha nduli aliyevamia kijijini
Mimi ndiye yule mwenye kifua cha chuma
Kifua kisichopitisha mkuki!
Kifua kisichopitisha risasi!
Mimi mpiganaji Nilikusanya askari wa jicho moja
Wakamkomesha mshenzi
Mimi nisiyeweza kuhangaishwa na vidudu mwitu!
Tazama – nikisema, nanguruma!
Sauti yangu inatetemesha ardhi!
Na vipofu wakajionea
Viwete wakasimama wakiwa mashujaa!
Usiku ulipoingia
Sauti yangu husababisha sisimizi wakasimama kwa miguu mitatu
Maajabu ya mwana makumbi!
|