SHAIRI : AMANI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI : AMANI (/showthread.php?tid=1980) |
SHAIRI : AMANI - MwlMaeda - 01-04-2022 SHAIRI NAWALETEA, HAKIKA KUWAIMBIA,
SIKIO KUNIPATIA, MENGI MKAYASIKIA,
AMANI YA TANZANIA, NA DUNIA NI SIKIA,
TUIDUMISHE AMANI, KWANI NI NGAO MUHIMU
HALI YA MTU YEYOTE, KUISHI BILA KUWASI,
HASA KWENYE MAMBO, YOTE AMANI INA NAFASI,
UCHUMI NA PANDE ZOTE, SIASA ISIYOASI,
TUIDUMISHE AMANI, KWANI NI GAO MUHIMU
AMANI KWENYE TAIFA, KATIKA NYANJA MUHIMU,
AMANI KWENYE TAIFA, KWAMBA MTU AHITIMU,
AMANI HAINA NYUFA, KUITUNZA SIO NGUMU,
TUIDUMISHE AMANI, KWANI NI NGAO MUHIMU.
AMANI HUVURUGIKA, YAKIWEPO MACHAFUKO,
DAMU NYINGI HUMWAGIKA, WATU WENGI HANGAIKO,
WANAWAKE HUDHURIKA, WAKUWA KAMA VIFUKO,
TUDUMISHE AMANI, KWANI NI NGAO MUHIMU
UROHO WA MADARAKA, BINAFSI CHANZO NDIO,
RAIA WAFEDHEHEKA, VIONGOZI HAO SIO,
HAWATAKI KOSOLEWA, WANAKUWA NI TISHIO,
TUIDUMISHE AMANI, KWANI NI NGAO MUHIMU
MAKUNDI YA UGAIDI, DUNIANI KWA JUMLA,
YANAFANYA MAKUSUDI, MACHAFUKO KUTAWALA,
UCHUMI NYUMA WARUDI, WADUMAA KAMA SWALA,
TUIDUMISHE AMANI, KWANI NI NGAO MUHIMU
UCHOCHEZI NAO SHIDA, UNAZUA MIGOGORO,
TAIFA LAWA HUSUDA, HUCHIMBWA KAMA MTARO,
AMANI YAFANYWA ODA, YAWEKOSA KAMA PAJERO,
TUIDUMISHE AMANI, KWANI NI NGAO MUHIMU
UDINI NA NI NJIA, YA KUONDOA AMANI,
UMAARUFU SIKIA, UTAWALA KUTAMANI,
MAKUNDI KUSHIKILIA, MACHAFUKO DUNIANI,
TUIDUMISHE AMANI, KWANI NI NGAO MUHIMU
YAFUATAYO TUMIA, ILI KULINDA AMANI,
UCHOCHEZI ACHILIA, UDINI KUTOTAMANI,
UGAIDI FUTILIA, TAIFA KULIDHAMINI,
TUIDUMISHE AMANI, KWANI NI NGAO MUHIMU
MWISHONI NIMEFIKIA, MENGI NIMESHAYATOA,
MENGINE YAWE USIA, KAZI MPATE TENDEA,
VIJANA KUZINGATIA, SHERIA KUSHIKILIA,
TUIDUMISHE AMANI, KWANI NI NGAO MUHIMU.
Na: Verian T. Francis (HKL-2018)
|