SHAIRI : KISWAHILI LUGHA YETU - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI : KISWAHILI LUGHA YETU (/showthread.php?tid=1976) |
SHAIRI : KISWAHILI LUGHA YETU - MwlMaeda - 01-03-2022 1:Kiswhahili lugha yetu,Lazima tuitunuku Shani tuipe mwakwetu,na maua tutunuku Lugha yenye ladha kuntu,Tuipambe kwa vikuku Tuipambe kwa vikuku,lugha yetu kiswahili 2:Lugha iliyosambaa ,Bara hata visiwani Lugha isiyo mawaa,tuipe yake thamani Watu waiongelelea,lugha hii yenye shani Tuipambe kwa vikuku,Lugha yetu kiswahili 3:Lugha iliyo thabiti,imeshika usukani Ni tamu kama matiti,ya mwana yu kifuani Lugha imejizatiti,Kutambaa duniani Tuipambe kwa vikuku ,Lugha yetu kiswahili 4:Maneno imesheheni,mabini na mabanati Mubashara na rosheni,sawia sasa ni kuntu Asante ikongoleni,Kiswahili chetu kuntu Tuiipambe kwa vikuku,Lugha yetu kiswahi 5:Beti tano zanitosha,Lugha yangu kuisifu Lugha mejaa bashasha,wanagenzi nawasifu Lugha yanifurahisha, siku zote naisifu Tuipambe kwa vikuku ,Lugha yetu kiswahili. mwl Mwenda Juhudi s.s |