SHAIRI : KA’NINGAKUWA RAISI, NINGESHITUWA DUNIYA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI : KA’NINGAKUWA RAISI, NINGESHITUWA DUNIYA (/showthread.php?tid=1969) |
SHAIRI : KA’NINGAKUWA RAISI, NINGESHITUWA DUNIYA - MwlMaeda - 01-03-2022 SHAIRI : KA’NINGAKUWA RAISI, NINGESHITUWA DUNIYA Raisi ningalikuwa, wa nchi ya Waswahili, ninajisikia kuwa, ningetowa yangu kali, wangu ulimi nikawa, nanena kula pahali, na n’kifika Marekani, hotuba kwa Kiswahili. ***** Kwa Wachina nikienda, ninawamba Kiswahili, kwa Warusi nikipanda, nao wafahamu hili, kula ya duniya kanda, n’getumia Kiswahili, wakalimani wakawa, wanafasiri hotuba. ***** Ningelonga kwa sitaha, na ufahari jameni, ugenini wakahaha, maso wakakodoeni, ino lugha ya madaha, n’geiwamba kwa makini, waelewe Afirika, nasi tunao ulimi. ***** Taswira itafakari, Ureno nimewasili, mabingwa wanahabari, wafuatia Kiswahili, ino ni lugha ya kheri, ‘ngefana kula pahali, ka’ningakuwa Raisi, ningeshituwa duniya. ******* Rwaka rwa Kagarama, Mshairi Mnyarwanda. |