MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI : SHATI BILA SARAWILI - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
SHAIRI : SHATI BILA SARAWILI - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6)
+---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50)
+---- Thread: SHAIRI : SHATI BILA SARAWILI (/showthread.php?tid=1962)

SHAIRI : SHATI BILA SARAWILI - MwlMaeda - 01-03-2022

SHAIRI : SHATI BILA SARAWILI
——————————-
1.
Amevala shati peke, lo ! sarawili hakuna,
atembeya kwa makeke, yeye hata soni hana.
Afanza kivyakevyake, siyo wa kuelewana,
kakifunika kifua, chini yu uchi wa nyama.

2.
Anaringia kusoma, shahada ya kuzamia,
na kimombo akitema, cha cheche za nadharia,
akidiriki kusema, jadiye aichukia,
mamboye ni ya majuu, alikotoka kushenzi.

3.
Ya ulaya ahusudu, kwa hayo amepagawa,
uzungu auabudu, ameisha kuulewa.
Kapata kizunguzungu, pasi hata kuelewa,
amevala shati peke, chini yu uchi wa nyama.

4.
Hajuwi shule ‘kienda, bila malezi ya baba,
kwa vidato atapanda, kiwa na kasoro wazi.
Ya kwao akiyaponda, wakati ndiyo mizizi,
chini yu uchi wa nyama, kavala tu kifuani.

5.
Usomi bila mizizi, yenye mashiko nyumbani,
ninawamba kwa uwazi, hujakusitiri chini.
Utaonekana chizi, ‘meehuka si utani,
weye umevala shati, hukuvala sarawili.

6.
Kusoma vema jamani, na pia kuna fanaka,
kama utakuthamini, nyumbani ulikotoka.
Inakuwa walakini, ya baba usiposhika,
utakuwa umevala, shati bila sarawili.

7.
Tena ukiwa shuleni, juwa unachosomea,
huko mbele maishani, uweze jitegemea.
Ya mafao yatamani, ya unyambi kukemea,
ili ‘sije ukavala, shati bila sarawili.

8.
Nakushukuru Jalia, fikara kunipatia,
aidha kun’saidia, tamati kuifikia.
Tungo ninamalizia, n’kiwa natumainia,
hadhira ‘meielewa, “shati bila sarawili.”

*****
Rwaka rwa Kagarama, (Mshairi Mnyarwanda,)
Jimbo la Mashariki,Wilaya ya Nyagatare,RWANDA