SHAIRI : HEKO DADA WA MWAMBAO - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI : HEKO DADA WA MWAMBAO (/showthread.php?tid=1961) |
SHAIRI : HEKO DADA WA MWAMBAO - MwlMaeda - 01-03-2022 SHAIRI : HEKO DADA WA MWAMBAO ************* 1. Naja leo jukwaani, jukwaa la washairi, Sifa kuwapatieni, akinadada mahiri, kwa mapishi namba wani, wajameni siyo siri, Heko dada wa Mwambao, mapishi yenu ya kwanza. 2. Ninaotaja Mwambao, ni pamwe na Visiwani, ni kwa Waswahili kwao, kwenye wadada makini, wana uta’lamu hao, wa upekee yakini, Heko dada wa Mwambao, mapishi yenu ya kwanza. 3. Haki hamna mfano, kwa upishi wenu nyie, anapinga nani hano? anene nimsikie, ni yupi analo neno, la kunikanusha mie? Heko dada wa Mwambao, mapishi yenu ya kwanza. 4. Na kama yangalikuwa, mashindano duniani, Waswahili wangekuwa, kwa mapishi namba wani, hii wote waelewa, wanaokujua Pwani, Heko dada wa Mwambao, mapishi yenu ya kwanza. 5. Hata pale ulifika, ustaarabu mbashara, wa Waswahili hakika, pande zetu huku bara, walizileta fanaka, pamwe na upishi bora, Heko dada wa mwambao, mapishi yenu ya kwanza. 6. Na siyo peke upishi, dada zetu ni wasafi, kwa bashasha na utashi, hukaribisha kwa safii, kwa matamu matamshi, aidha sauti safi, Heko dada wa Mwambao, mapishi yenu ya kwanza. 7. Tungo ninakamilisha, tuzo nikiwapatia, ni taji ninawavisha, taji la umalikia, na awagee maisha, ya kheri wetu Jalia, Heko dada wa Mwambao, Mapishi yenu ya kwanza. ************ Rwaka rwa Kagarama, Mshairi Mnyarwanda. Jimbo la Mashariki, Wilaya ya Nyagatare, RWANDA. |