SHAIRI : KI’MZINYI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI : KI’MZINYI (/showthread.php?tid=1958) |
SHAIRI : KI’MZINYI - MwlMaeda - 01-03-2022 SHAIRI : KI’MZINYI ————- 1. Hodi hodi na salamu, wa ushairi Mamwinyi. N’na wasaili kwa hamu, wenye jawabu ni nyinyi. Miye msinilaumu, akina Gakurya Mwinyi. Mengi sijayang’amua, hebu nifundeni ninyi. 2. Hususan pwani huko, Kiswahili kulikoni. Yaliko yake mashiko, na mizizi’ye kwa ndani. Lahaja nyingi ziliko, kama vile Kibajuni. Jamani huko mliko, Ki’mzinyi lahaja gani? 3. Kiswahili lugha tamu, kinazo nyingi lahaja. Mathalani kihadimu, Kingwana na kiunguja. Ninakipata kiamu, Kimgao na Kingadzija. Ki’mzinyi mwafahamu, ya wapi hii lahaja? 4. Chibalonzi na Kimvita, Chimiini na Kimwani. Kingozi na Kimtang’ata, nazielewa makini. Hino lahaja ni tata, jama nitatulieni. Ki’mzinyi wapi n’tapata, mana’ye hii lahaja? 5. Zipo zingine lahaja, ni nyingi za Kiswahili, Miye yangu moja haja, nijuzeni jambo hili. Wasanii tu wamoja, nipeni yenu kauli. Ki’mzinyi ni lahaja, ya cha nani Kiswahili? 6. Subukhana shukurani, tamati ‘menifikisha. Ya ushairi makini, hoja umepeperusha. Baraka wajalieni, pia kuwaneemesha. Wote hapa Kisimani, wape maisha marefu. ***************************** Rwaka rwa Kagarama, (Mshairi Mnyarwanda) Jimbo la Mashariki, Wilaya ya Nyagatare,RWANDA. rwakakagarama2020@gmail.com |