SHAIRI : NIANZE NA NINI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI : NIANZE NA NINI (/showthread.php?tid=1956) |
SHAIRI : NIANZE NA NINI - MwlMaeda - 01-03-2022 Nimekunjato miguu, na mwili u tuli chini Ba’da kupata nafuu, kwa tabu za maradhini Nautunga wimbo huu, nambe nianze na nini? Ni shura ya mimi nawe, nyongo mkaliya ini Fikira zako zituwe, upimeto kwa makini Nachotaka niambiwe, kwako nianze na nini? Kama nianze na gari, sema ya aina gani Lolote nipo tayari, benzi na isuzu jani laazizi nishauri, kwako nianze na nini? Ama nianze na nyumba, utakuwa furahani Kwa wengine utatamba, kodi haulipi sini Muhibaka nakuomba, nambe nianze nini? Sema nianze na ndoa, kama kwako ndo amani Ili nisikupe doa, ipande yako thamani Kwa vyovyote nipo poa, nambe nianze na nini? Hata kama utakalo, kwenye shairi huoni Nambe nilifanye hilo, ewe wangu wa moyoni Nataka neno ambalo, lasema nanze na nini? Mwisho nafunga kauli, mjue muomba nani Mwana wa mzee Ali, ambaye Moa nyumbani Moto wenu Abtali, ambwaye Tanga mgeni MBARUKU ALLY MOTO WENU ABTALI MJAALA 0717199835 01/05/2019 Nikiwa Kigogo Dsm Mzaliwa Moa Tanga |