MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI : DHANA YA KAZI - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
SHAIRI : DHANA YA KAZI - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6)
+---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50)
+---- Thread: SHAIRI : DHANA YA KAZI (/showthread.php?tid=1953)

SHAIRI : DHANA YA KAZI - MwlMaeda - 01-03-2022

SHAIRI : DHANA YA KAZI
********
1.
Ninaitunga nudhumu, fikira niweke wazi,
kwa shairi maalumu, lenye wasifu wa kazi.
Bariki hili jukumu, Mpaji Mungu Mwenyezi,
dhana ya KAZI dhimaye, jama haina kifani.
2.
Anga n’napoivinjari, ya fikira za utunzi,
KAZI n’kiitafakari, kuhitimisha siwezi.
Hata kinache nakiri, ngumu kupigia mbizi,
dhana ya KAZI dhimaye, jama haina kifani.
3.
Siwezi pata maneno, yote kwa dhima ya KAZI,
hata kiwango cha wino, kuandika sifa hizi.
Ninafikiria mno, wasifu we simalizi,
dhana ya KAZI dhimaye, jama haina kifani.
4.
KAZI ni yetu mirathi, mtu kamili ajuwa,
tangu ndemi na mathathi, enzi z’Adamu na Hawa.
Imani tulizorithi, mwanya mkubwa yagewa,
dhana ya KAZI dhimaye, jama haina kifani.
5.
Ni ya Kiswahili haya, tulikuwa tukifundwa,
“Usione vyaelea, vinakuwa vimeundwa”.
Kazi ‘sipozingatia, maishani utashindwa,
dhana ya KAZI dhimaye, jama haina kifani.
6.
Ya binadamu thamani,, haipimwi kwa suraye,
si urefuwe jameni, au kwayo maguvuye.
Ni KAZI akithamini, ndo huthamanika naye,
dhana ya KAZI dhimaye, jama haina kifani.
7.
MpendaKAZI hupatana, wivu na uvivu hana,
yeye hanazo fitina, wala mambo ya hiyana.
Huyo ni wa kufaana, siyo wa kufarakana,
dhana ya KAZI dhimaye, jama haina kifani.
8.
Na maisha bora huwa, yanapotendewa KAZI,
na wana nao hukuwa, na desituri ya KAZI.
Tajiri nchi ikiwa, watuwe watendaKAZI,
dhana ya KAZI dhimaye, jama haina kifani.
9.
Wa jamii ukombozi, si lelemama ku’pata,
hadi ufanyiwe KAZI, hata ikibidi vita.
Ikipuuziwa KAZI, matokeoye kujuta,
dhana ya KAZI dhimaye, jama haina kifani.
10.
Na ba’da ya ukombozi, wa siasa hususan,
huendelezwa na KAZI, uchumi kuukuzeni.
Uno msingi lazizi, wa m’endeleo yakini,
dhana ya KAZI dhimaye, jama haina kifani.
11.
Inatajwa mara nyingi, mu vitabu vya wajuzi,
kwa tenzi na visa vingi, na khutba za welekezi.
KAZI wasifuwe mwingi, kuumala siviwezi,
dhana ya KAZI dhimaye, jama haina kifani.
12.
Beti nazitamatisha, thenashara zimetimu,
tungo aloniwezesha, namshukuru Karimu.
Kwa hadhira n’peperusha, Asalam’aleikumu,
dhana ya KAZI dhimaye, jama haina kifani.

************
Rwaka rwa Kagarama, Mshairi (Mnyarwanda),
Jimbo la Mashariki, Wilaya ya Nyagatare, RWANDA.