SHAIRI : KUMBE NANGOJWA NISEME - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI : KUMBE NANGOJWA NISEME (/showthread.php?tid=1949) |
SHAIRI : KUMBE NANGOJWA NISEME - MwlMaeda - 01-03-2022 Heri hapa nipahame, nirudi kwetu wenzangu Nikalishe nikalime, nikafinyange na vyungu Lakini musinipime, kutaka undani wangu Kumbe nangojwa niseme, nipashwe vidonge vyangu Ni kimya sitolalama, nilonalo siwambii Bora nirudie nyuma, ingawa siyakimbii Naitafuta salama, ninaradhiwa kudhii Kumbe kwa kutokusema, pia haisaidii Kila nikiyaungama, yasiwe mambo ya ngumi Wao wakiniandama, kunisingizia mimi Hudhania yatazima, kwa kuufyata ulimi Kumbe wao watasema, ingawa mimi sisemi Wao wananizingira, wanibanangia boma Napigwa kama mpira, waniteka wanizoma Siwafanyii hasira, ingawa yananichoma Naamuwa kuwazira, watajibiwa na koma Hapa najifanya bubu, sineni wanganinena Najitoa taratibu, haya si ya nyemi tena Nacha zipande ghadhabu, tuanze kujibizana Wakisema niwajibu, ibaki kutukanana Mohamed Khamis Takaungu 03.04.2019 |